Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Mstaafu
Joseph Warioba (kushoto) akiongea na Mawaziri wa Katiba na Sheria kutoka
Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Mathias Chikawe (kulia) na Abubakar Khamis
Bakari (kulia kwa Jaji Warioba) nje ya ofisi za Tume mara baadaya Mawaziri
kutembelea ofisi za Tume leo. Katikati Naibu wa
Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki na wengine ni watendaji kutoka Tume
na Wizara za Katiba na Sheria (Picha na Tume ya Katiba).
Mkuu wa Kitengo cha Taarifa Rasmikatika Tume ya Mabadiliko ya Katiba Hanifa
Masaninga (kushoto) akitoa maelezo jinsi sauti zenye maoni ya wananchi
zilizorekodiwa mikoani zinavyofanyiwa kazi, akitowa maelezo hayo kwa Mawaziri wa Katiba na Sheria
kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano, MathiasChikawe (kwa pili kulia) na
Abubakar Khamis Bakari wa Serikali ya MapinduziZanzibar (watatu kushoto) na
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki(kulia). Wa pili kushoto ni
Katibu wa Tume Assaa Rashid
Mkuu wa Kitengo cha Utafitikatika Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mohammed Khamis
Hamad (kulia) akiwaelezajinsi maoni ya wananchi yanavyopokelewa kutoka katika
mitandao ya kijamiiMawaziri wa Katiba na Sheria kutoka Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Bw.AbubakarKhamis Bakari (kushoto), Bw. Mathias Chikawe kutoka
Serikali ya Jamhuri yaMuungano na Naibu wake Angellah Kairuki
Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (TEHAMA) katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba Shaaban Chum (kushoto) akiwaeleza Mawazir i wa Katiba na Sheria kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Abubakar Khamis Bakari (wa pili kulia) na wa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano, Mathias Chikawe (wa pili kushoto) na Naibu wake
Angellah Kairuki. Mwingine ni Katibu wa Tume Assaa Rashid
danganya wazanzibari hio , wenye macho wameona , muungano hautakiwi hata mkijidai kuwapa huo ukuu wa vitengo vyote kama mnayvoonyesha kwenye hizo picha akina mohamedi na shabani na hanifa , hamuwezi kuwahadaa wenye akili
ReplyDeleteenyi akina shabani , mwamedi and hanifa, tambueni kuwa mnatumiwa na watanganyika kutengeneza katiba wanayoitaka wao , mjue haki za waznz ziko mikononi mwenu na mtaziuza , kwa mwangalio wangu nyote dhaifu hamna uwezo wa kusema hata kwi! Huenda mkafaidika kutokana na hili lakini ni kuwa muda tu ambao mtakuwepo hapa duniani , siku mtakayoonana na Mola wenu ndipo mtajua yale mliyoyafanya na kuyasimamia , ukumbusho utawafaa wenye kuzingatia
ReplyDelete