Habari za Punde

Mkutano wa Kupitia Sera ya Habari Zanzibar Bwawani.

 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Bihindi Hamad, akifungua Mkutano wa kupitia Sera ya Habari Zanzibar, ulioandaliwa na Tume ya Utangazaji Zanzibar na kuwashirikisha Viongozi wa Vyombo vya Habari Zanzibar vya binafsi na vya Serekali uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani,
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Utangazaji Zanzibar Chande Omar, akitowa maelezo kuhusu upitiaji wa Sera ya Habari Zanzibar wakati wa Ufunguzi wa Mkutano huo uliofunguliwa na Naibu Waziri wa Habari Zanzibar Bihindi Hamad.  

 Muwezeshaji Ali Rashid akitowa mada ya kuhusu vyombo vya habari Kuelimisha Jamiina kuwapa Habari za Kila Siku zinazotoke,
 Mkurugenzi wa ZBC Redio Rafii Haji, akiwasilisha Mada ya Utangazaji wa Umma kwa Vyombo vya Habari Zanzibar kutoka Analogi kwenda Digitali, katika Mkutano wa kupitia Sera ya Habari Zanzibar, ilioandaliwa  na Tume ya Utangazaji Zanzibar.    
 Muwezeshaji Suleiman Seif, akiwasilisha Mada ya Ukuwaji wa Uchumi na Utamaduni Mila naSilka, akitowa mada yake katika mkutano wa kupitia Sera ya Habari Zanzibar.
 Wadau wa Vyombo vya Habari Zanzibar wakifuatilia Mada zinazotolewa na watoa mada kupitia Sera ya Habari Zanzibar  na kuwashirikisha Wadau wa Vyombo vya Habari Binafsi na vya Serekali ilioandaliw na Tume ya Utangazaji Zanzibar na kufadhiliwa na UNESCO.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) Hassan Mitawi akitowa Mada katika Mkutano wa kupitia Sera ya Habari Zanzibar, ilioandaliwa na Tume ya Utangazaji Zanzibar. 
 Kamishna wa Michezo na Utamaduni Zanzibar Bakari Hamad Mshindo akichangia mada katika mkutano huo, zilizotolewa na watoa mada kuhusu Sera ya Habari Zanzibar.  
Mdau wa Habari Zanzibar  Hamza Rijali, akichangia mada zilizowasilishwa katika Mkutano wa kupitia Sera ya Habari Zanzibar ilioandaliwa na Tume ya Utangazaji Zanzibar na kufadhiliwa na UNESCO, katika ukumbi wa hoteli ya bwawani. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.