Habari za Punde

Uokoaji maiti zilizofukiwa mgodini wakamilika

Na Mwandishi wetu
ZOEZI la kufukua maiti saba za watu waliofunikwa na kifusi katika machimbo ya madini katika Kata ya Nandagala Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi limekamilika asubuhi ya jana.

Diwani wa Kata Ruangwa,Andrew Chikongwe alibainisha kuwa kazi ya kufukua kifusi hicho imechukua muda mrefu kufuatia na kuwepo kwa zana duni za kufukua mchanga hali iliyofanya kazi hiyo kuwa ngumu.

Chikongwe aliwataja Mmrehemu hao ni Nyang'ana Mkelecha, mkazi wa Musoma,Mohamed Omari Fondogoro,mkazi wa Morogoro, Bakari Liganga mkazi wa Chunyu Ruangwa,Rajab maarufu Roger mkazi wa Musoma,Uwesu Bakari Abeid mkazi wa Rondo,Chakoda mkazi wa Dar es Salaam na Rashid Ally maarufu Bade mkazi wa Masasi mkoani Mtwara.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.