Habari za Punde

Dk Bilal afungua mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ay CCM

 Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Tifa ya CCM Dr. Mohd Gharib Bilal akiingia katika ukumbi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kiliopo Dodoma akiongozwa na Kaimu Mwenyekiti wa Wazazi Taifa Bibi Amina Mabrouk.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Mh. Pius Msekwa kulia yake ni Mke wa Makamuj wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi na Katibu Mkuu wa Wazazi Taifa Nd. Dadi Suleiman Dadi wakishangiria vifijo vilivyoanikiza ndani ya Ukumbi wa Bwalo la Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kiliopo Mjini Dodoma wakati wa Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Wazazi Taifa. Mkutano huo ulifunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mohd Gharib Bilal.

Na Othman khamis Ame

Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi ina wajibu wa kuzingatia na kutafuta namna ya njia bora itakayosaidia mbinu sahihi za kupambana na mmong’onyoko wa maadili hasa kwa Vijana hapa Nchini.
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muuungano wa Tanzania Dr. Mohd Gharib Bilal alisema hayo wakati akiufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya ya Wazazi Taifa uliofanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Kiliopo nje kidogo ya Mji wa Dodoma.


Dr. Bilal alisema Mmong’onyoko wa Maadili unaoonekana kutapakaa kila siku umekuwa changamoto kubwa inayoikabili Jumuiya hiyo ambayo ndio muhusika Mkuu wa ulinzi wa Maadili hayo.
 
Alieleza itapendeza kwamba ndani ya Jamii katika kukabiliana na suala hilo zito Mzazi mmoja mmoja pekee atawajibika katika kuhakikisha anaendelea kuwa na Tabia njema kuanzia mavazi, kauli na hata vitendo vyake vya kila siku.
 
Dr. Bilali alifahamisha kuwa Wazazi bado wanakabiliwa na jukumu kubwa la kuhakikisha Jamii inayowazunguuka inaendelea kubaki katika hali ya amani na usalama wakati wote.
 
Akizungumzia suala la Uchaguzi wa Jumuiya hiyo Dr. Bilal aliwataka Viongozi wa Jumuiya hiyo ya Wazazi kuhakikisha wanaondoka Dodoma wakiwa na Jumuiya iliyopata Viongozi mahiri na madhubuti wa kuweza kukabiliana nc changamoto zilizopo.
 
Alisema hatua hiyo itapatikana iwapo wanachama watakaowachaguwa kuwa Viongozi wao watajikubalisha kuwa karibu na wanaowaongoza sambamba na kuheshimu taratibu ambazo chama tayari imeziweka.
 
Aliwatahadharisha wajumbe hao kujiepusha na rushwa ambayo inaonekana kuvuruga maadili na kanuni za uchaguzi ndani chama pamoja na Jumuia zake.
 
“ Anayetoa fedha kwa kutafuta madaraka kwa kweli hana nia njema na hatma ya kuwaongoza wenzake”.Alitahadharisha Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Dr. Bilal.
 
Dr. Mohd Gharib Bilal alizitaja Siasa za zama zilizopo hivi sasa kuwa zimebadilika kiasi kwamba Uongozi wa Jumuiya ya Wazazi unapaswa kuzingatia kwa makini siasa hizi ambazo wanawajibika kukabiliana nazo katika utendaji wao.
Kuhusu uwekezaji Dr. Bilal aliutaka Uongozi wa Wazazi kuongeza nguvu za ziada katika uwekezaji vitega uchumi kwa lengo la kujiendesha wenyewe bila ya kusubiri nguvu za Chama au wafadhili.
 
Alisema Jumuiya ya Wazazi ilikuwa na Vitega uchumi vingi kipindi ilipoanzishwa lakini hivi sasa inaonekana kupoteza sifa zake hizo jambo ambalo inakuwa katika mazingira magumu kiuendeshaji.
 
Mapema Makamu Mwenyekiti akiwa pia Kaimu Mwenyekiti ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi Taifa anayemaliza kipindi kilichopita Bibi Amina Mabrouk alisema yapo mafanikio makubwa ndani ya Jumuiya hiyo tokea ilipoamua kutekeleza mikakati iliyojipangia ya kujiendesha Kiuchumi.
 
Bibi Amina alisema uanzishwaji wa Benki Familia { Family Bank } ni moja ya mafanikio hayo inayochangia mapato zaidi kufutia wanafunzi wanaosoma katika skuli za Wazazi kulipa ada zao moja kwa moja kupitia Benki hiyo na kupunguza uvujaji wa mapato.
 
Hata hivyo Bibi Amina Mabrouk alizitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili Jumuiya hiyo ya Wazazi Taifa ikiwa ni pamoja na ukosefu wa hati miliki ya majengo yake mbali mbali yakiwemo skuli.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.