Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna (wamwanzo kulia)akitoa hotuba katika sherehe za kukabidhiwa Madarasa 17yaliofanyiwa Ukarabati pamoja na Madawati180 yaliotengenezwa ikiwa ni msaada kutoka Shirika la Maendeleo la KOICA kutoka Korea,kwa ajili ya Skuli ya kukabidhiwa Madarasa 17yaliofanyiwa Ukarabati pamoja na Madawati180yaliotengenezwa Chuini ilio kaskazini Unguja kushoto yake ni Meneja wa Shirika la KOICA Seung Beom Kim.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna akimkabidhi Cheti cha Shukurani na Ushirikiano Meneja wa Shirika la KOICA kutoka Korea Seung Beom Kim.katika Hafla ya Sherehe za kukabidhiwa Madarasa 17yaliofanyiwa Ukarabati pamoja na Madawati180yaliotengenezwa na Shirika hilo kwa ajili ya Skuli ya Chuini ilio kaskazini Unguja
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Ali Juma Shamhuna (Kushoto)akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Abdalla Mzee Abdalla katika Sherehe za kuwatunuku vyeti Walimu wanaofundisha Somo la Kingereza waliomaliza Mafunzo yao ya kuwajengea Uwezo wa kutumia Lugha hio katika Ufundishaji hapo Kituo cha Walimu cha Taifa Nkruma
Mwalimu Salum Omar kutoka Skuli ya Machui Zanzibar akionyesha namna ya kuwafundisha Watoto Somo la Kingereza kwa Kutumia Kingereza na mbinu mbalimbali za Usomeshaji walizojifunza katika mafunzo yao yaliochukua muda wa siku 20 hapo Kituo cha Walimu cha Taifa Nkruma.
Mwalimu Teresia Husein kutoka Skuli ya Kibele Zanzibar akionyesha namna ya kuwafundisha Watoto Somo la Kingereza kwa Kutumia Kingereza na mbinu mbalimbali za Usomeshaji walizojifunza katika mafunzo yao yaliochukua muda wa siku 20 hapo Kituo cha Walimu cha Taifa Nkruma. Picha zote na Yussuf Simai, Maelezo
No comments:
Post a Comment