Habari za Punde

Lini na Sisi...

Dear Zanzibaris,

 After reading the below story, I am asking a question to myself that is which Government has financed the project and why our Government has not thought to look into constructing such transportation on both the Islands of Unguja and Pemba.

I am sure such a project is viable and Tanzanian Government is there to help Zanzibar reduce the transportation problems we have.

At the same time our roads are becoming congested and it keeps on claiming lives through accidents.

I am suggesting that those responsible should look into this issue of constructing railway services both on Unguja and Pemba Islands to help our people. IT CAN BE ACHIEVED

Tuesday, October 30, 2012


Usafari wa reli Dar rasmi


Dk Mwakyembe kufukuza wafujaji

Na Kunze Mswanyama,Dar es salaam

NDOTO ya muda mrefu waliyokuwa nayo wakaazi wa jiji la Dar es salaam ya kuondokana na kero ya kugombania daladala,lugha chafu za makondakta,msongamano wa magari barabarani na daladala kujaza abiria kupindukia uwezo wake, hatimae imetimia jana baada ya usafiri wa treni kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison Mwakyembe.

Mapema Septemba,Dk.Mwakyembe aliwaahidi wakaazi wa jiji hilo kuwa iwe isiwe katika kipindi cha awamu ya nne lazima usafiri huo uanze ndani ya mwezi Oktoba jambo ambalo limetimia jana.

”Serikali ya CCM inawasikilza wananchi na kuwatafutia ufumbuzi wa matatizo yao,” alijinadi Dk.Mwakyembe.

Treni hiyo itakuwa ikianzia safari zake kutoka kituo chake hadi Ubungo Maziwa ambapo itahudumia abiria zaidi ya 900 kwa safari moja huku kila mmoja akitozwa shilingi 400 tu kwa safari moja itakayochukua muda wa dakika 40.

Akizindua usafiri huo uliogharimu shilingi bilioni 5 kwa kukarabati mabehewa 14, injini mbili na kutengeneza mataruma ya reli, Dk.Mwakyembe alisema atahakikisha chini ya uongozi wake treni hiyo inafanya kazi bila kusimama ili kuokoa fedha za Watanzania zinazopotea kwenye foleni za barabarani.

Uchunguzi uliofanywa na taasisi kadhaa nchini, zilibaini kuwa zaidi ya shilingi bilioni 4 hupotea kila siku jijini kutokana na foleni jambo linalowafanya wakaazi hao kuchelewa kwenye biashara na shughuli zingine za kiuchumi.

“Kwanza nawapongeza mafundi wazawa wote mlioshiriki kurekebisha kila kitu hadi treni kupita juu ya reli hii. Mmeokoa fedha nyingi sana maana tulitenga fedha kukodi mabehewa toka India ambapo kwa siku hugharimu milioni tatu kwa behewa hebu piga hesabu kwa mwezi ni shilingi ngapi lakini mmefanya yote hayo kwa bilioni 5 tu,” alisema Mwakyembe.

“Tulitaka kukodi mabehewa 18 na injini zake,nyinyi mmerekebisha haya 14 kwa shilingi bilioni 2.4 na shirika la Rahco wametengeneza reli kwa gharama ya bilioni 2.6,mmeokoa fedha nyingi sana,tutahakikisha wanafanya kazi hadi Jumamosi ila Jumapili na siku za sikukuu wapumzike,” alitamba Dk. Mwakyembe.

Waziri huyo pia aliwataka wananchi waliojenga nyumba za biashara na za kuishi kwenye hifadhi ya reli kuondoka mara moja kwani wanahatarisha maisha yao na ya watumiaji wa treni na kuahidi kutumia sheria kuwaondosha kwenye hifadhi hiyo.

Akizungumzia malalamiko ya baadhi ya watumishi wa shirika hilo kuhusiana na malipo yao, Dk. Mwakyembe alisema:”Acheni kulalamika tu kwenye risala zenu niiteni kama mna matatizo na kama malalamiko yapo hata mimi nawalalamikia nyinyi kwa wizi wa mafuta ya treni na shaba kwa kutumia treni hii hii.”

“Kama wewe unanung’unika kila wakati kamnung’unikie mke wako kwanza ndipo uje kwetu maana kila mmoja akilalamika itakuwaje mimi nawataka muache wizi wa mafuta ili tutatue ya kwenu tena mmebuni njia mbadala ya wizi sasa mnatumia treni kuiba shaba,ni hatari kweli,” alisema.


Aliitaka menejimenti ihakikishe inawabadilisha mawazo wakaazi wa jiji walioamua kugeuza reli kuwa dampo kwani inaleta picha mbaya hasa kwa wageni watakao kuwa wakitumia usafiri huo.

Aidha alibainisha changamoto walizozibaini kuwa ni pamoja na kila kituo, treni itasimama kwa dakika moja badala ya mbili za awali, ambapo wasimamizi watreni watafunga mlango mara baada ya honi kupigwa. Alisema abiria wanapanda treni kwa kupanga mistari badala ya kugombania.

Waziri huyo asiye na kawaida ya kumung’unya maneno,aliwataka wafanyakazi wote wenye nia ya kulihujumu shirika hilo kujiengua mara moja badala ya kusubiri kufukuzwa ili wabaki wenye nia njema na nchi.

“Kama hutaki kubadilika acha kazi sasa hivi kwa sababu wapo vijana wengi tu mitaani wenye elimu nzuri nitawaleta asubuhi tu msitubabaishe jamani na nitahakikisha namwondoa yeyote atakayeleta hujuma kwenye shirika hili,” alisema.

Pia aliwataka watumishi hao kujua kuwa wao ni tegemeo la serikali kwani wamefanya kazi kubwa ambayo kama ingefanyika nje ya nchi ingegharimu kiasi kikubwa cha fedha hivyo wajue serikali yao
inawathamini.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Nchini (TRL), Injinia Kipallo Kisamfu,alimwambia Waziri kuwa gharama kubwa za uendeshaji haziendani na hali halisi ya soko huku pia usalama wa abiria na treni ukiwa shakani kutokana na wananchi kuingilia hifadhi ya reli na kujenga
makazi.

“Tulipendekeza nauli iwe shilingi 800 kwa abiria lakini tumeambiwa tutoze 400 tu hivyo bado haitakidhi mahitaji yetu maana tulidhamiria kutumia lita 3 kwa kilomita lakini tutafanya kazi hivyo hivyo,” alisema.

Pia aliwahimiza wananchi kujitokeza kuutumia usafiri huo wa uhakika ambapo hautawachosha kwani ni dakika 40 tu watakuwa wamefika Ubungo.

Mwanzoni mwa utawala wa awamu ya tatu,aliyekuwa waziri wa usafirishaji, Prof.Mark Mwandosya aliwahi kujaribisha usafiri huo lakini hakufanikiwa kutokana na changamoto nyingi alizokumbana nazo ikiwani pamoja na uhaba wa fedha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.