Habari za Punde

Maalim Seif kuzungumza na Wanahabari kesho

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, kesho anatarajiwa kuzungumza na wahariri wa vyombo vya habari nchini juu ya mambo mbali mbali ya kitaifa yakiwemo mafanikio na changamoto zinazoikabili Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, mkutano huo utafanyika hoteli ya Zanzibar Grand Palace iliyopo Malindi mjini Zanzibar mnamo majira ya saa nne asubuhi.
Taarifa hiyo imesema ajenda nyengine zitakazojadiliwa katika mkutano huo wa kawaida ni pamoja na changamoto za upatikanaji wa vitambulisho vya mzanzibari mkaazi, pamoja na mchakato wa utoaji wa maoni juu ya mabadiliko ya katiba mpya ya Tanzania.
Hassan Hamad (OMKR)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.