Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA Vuai M Suleiman, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uandikishaji wa Vitambulisho vya Taifa unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo katika Visiwa vya Zanzibar, kuazia 15-10-2012, na kuchukua siku kumi kila Wilaya kuandikisha Wananchi wa Wilaya hizo, ili kila Mwananchi awe amejiandikisha kupata fursa hiyo, na hakuna mwananchi atakayekosa kuandikishwa ili kupata Kitambulisho cha Taifa.mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Walemavu Welesi.
Waandishi wa habari wakiwa katika Mkutano na Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa Zanzibar Vuai M.Suleiman, akitowa maelezo ya kuaza kwa andikishaji wa Vitambulisho vya Zanzibar.
Mwantanga Ame akiuliza kutokana na uandikishaji huuhausiani na Dini wala Kisiasa jee?mmetowa elimu kwa Viongozi wa Dini na Siasa kuhusiana na undikishaji huu tayari mmeshatowa elimu kwa viongozi hao kuhusiana na zoezi hilo la Vitambulisho.na kuhusu sheria ya NIDA inasemaje kuhusu uandikishaji wa kupata kitambulisho cha Taifa.
Mzee Mwakenja akitaku kupata ufafanuzi kuhusu utaratibu wa Uandikishaji wa Vitambulisho.
Khatib Suleiman ametaka kujuwa umri halali wa kupata kitambulisho na vigezo vitakavyotumika katika uandikishaji kwa Wananchi wa Zanzibar.
Mwandishi Mkongwe wa habari Said Salim, ametaka kujuwa Uandikishaji huu wa Vitambulisho mmejifunza vipi katika uandikishaji na kila mzanzibar atapata kitambulisho, au itakuwa kama kitambulisho cha mzanzibar watu wengi wamekosa vitambulisho kwa kukosa sifa.na mtatumia miaka ya kuzaliwa ya kiarabu maana kuna baadhi ya watu hutumia miaka ya kuzaliwa ya kiarabu hapa zanzibar.
No comments:
Post a Comment