Habari za Punde

Zaidi ya Vijana 85 Wajitokeza Kujuwa afya zao.

Muwezeshaji wa Jumuiya ya ZAYEDESA, Msimamizi wa Kituo cha Ushauri Miembeni,Bakari Shamte. akihamasisha Vijana wakati wa kuonesha cinema kuhusiana na athari za matumizi ya Dawa za Kulevya na Maambukizo ya Ukimwi kwa Vijana, maonesho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Mafarasi Kiwengwa Mkoa wa Kaskazini Unguja.

 Zaidi ya Vijana 85 wa Wamejitokeza kupima Afya Zao..

Zaidi ya Vijana 85, wamejitokeza kupima ili kujuwa afya zao katika kijiji cha Kiwengwa Mafarasi,wakati wa kutowa ushauri nasaha kwa vijana wanaojishughulisha na biashara katika sehemu hiyo, wamehamasika na ujio wa Vijana wa Jumuiya ya ZAYEDESA, kutowa elimu ya maambukizo ya UKIMWI kwa vijana katika Zanzibar.

Vijana hao wamehamasika na Ushauri na elimu walioipata kupitia njia ya Cinema na Ushauri nasaha uliokuwa ukitolewa na Vijana hao walipokuwa wakipita katika sehemu mbalimbali za eneo hilo na kutowa elimu hiyo kwa vijana na kuhamasika kujitokeza kupima afya zao kujijuwa na kuwa na uhakika wa afya zao na kuendelea na kujikinga dhidi ya maambukizo ya UKIMWI.

Baadhi ya Vijana hao walikuwa na wasiwasi wa kujitokeza kupima afya zao kutokana na kuogopa matokeo ya majibu ya vipimo vyao kutokana na kukosa ushauri na woga waliokuwa nao vipi watapokea majibu na jamiiiytawaonaje.

Wamesema ujio wa Vijana wa ZAYEDESA katika eneo lao ni moja ya faraja waliopata na kuwa na matumai ya kuishi kwa kujuwa afya zao na kuwataka vijana wezao kujitokeza na kwenda sehemu husika kupata elimu juu ya  maambukizo ya ukimwi nma jinsi ya kujikinga na janga hilo.

Mmoja wa Kijana aliejitokeza kujuwa afya yake amefarijika kupata majibu mazuri na ataendelea kujitunza  na kutumia njia anayotumia katika kuchukuwa tahadhari na maambukizo ya ukimwi na kuwaasa vijana wezake kujitoeza katika vituo vya afya kupima na kujuwa afya zao ili kuwa na matumaini ya maisha yao juu ya maambukizo ya ukimwi.

Amesema yeye alikuwa na wasiwasi juu ya afya yake lakini sasa wasiwasi umemtoka baada ya kupima na kujitambuwa kama yoko safi na ataendelea kujilinda na atakuwa mwalimu kwa vijana wezake.

Nae Ofisa wa Mipango wa  Elimu ya Ukimwi katika ZAYEDESA Mgoli Lucian, amefarijika na mwiitikio wa Vijana wa eneo hilo la Kiwengwa Mafarasi kwa kujitokeza kwa wingi katika kupata ushauri Nasaha na kupima afya zao.

Amesema vijana wa eneo hilo mameitikia wito wao baada ya kupata elimu juu ya matumizi ya dawa za kulevya jinsi inavyochangia maambukizo ya ukimwi kwa vijana wakati wa kuchangia shindao wanazotumia kuazimana.

Ametowa shukrani wa Sheha wa Kiwengwa kwa ushirikiano wake jinsi ya kuwahamasisha vijana wa eneo hilo na kuitikia wito huo na kujitokeza kiasi hicho cha Vijana 85 katika eneo hilo.
Msimamizi wa Kituo cha Ushauri Nasaha  Miembeni Bakari Shamte, akitowa ushauri wa maambukizo kwa Vijana wanaotumia dawa za kulevya jinsi ya athari zake wanazopata Vijana.



 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.