HOTUBA YA MKURUGENZI
WA MAMLAKA YA VITAMBULISHO VYA TAIFA OFISI YA ZANZIBAR, KWA WAHARIRI NA
WAANDISHI WA HABARI ZANZIBAR 03/10/2012
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA. Vuai Mussa Suleiman.
Ndugu
Wahariri na waandishi wa habari
Maafisa
toka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Mabibi
na Mabwana,
Assalamu - alaykum
Utangulizi
Awali
ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutuwezesha kukutana hapa tukiwa na
afya njema katika kushirikishana hatua muhimu katika utekelezaji wa jambo
muhimu la kihistoria katika mustakabali wa Nchi yetu,kwa kuanza mchakato wa usajili
na Utambuzi wa watu, unaolenga hatimaye kutoa vitambulisho vya Taifa.
Ni wazi
wazo la kuwa na Vitambulisho vya Taifa limechukua muda mrefu sasa na kwa muda
mrefu serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha kuwa jambo hili linakamilika na
mchakato unaanza. Na leo ndugu wanahabari, naomba kuwajulisha Usajili wa
wananchi kwa upande wa Zanzibar unaanza rasmi 15/10/2012 baada ya kukamilika
kwa usajili wa watumishi wa Umma.
Kwa hakika tuna kila sababu ya kuipongeza
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na kwa namna ya pekee, sekikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais wetu Mheshimiwa Ali
Mohamed Shein. Kwa hakika jitihada kubwa mlizozifanya kuhakikisha mradi huu
unafanikiwa na kutekelezeka mnapaswa kupongezwa.
Ndugu
Wanahabari,
Zanzibar tunakusudia kuanza shughuli ya
usajili na utambuzi wa Watu rasmi kama hakutakuwa na mabadiliko yeyote tarehe
15/10/2012 na utaratibu tuliojiwekea ni kusajili kiwilaya na kila Wilaya
imepangiwa siku 10 za usajili.
Ni imani yangu kubwa wananchi, Viongozi
wa dini, masheha na wanasiasa kwa jumla, tutatoa ushirikiano kwa maafisa wetu
wasajili ambao watakuwa katika kila shahia kufanya usajili, na kila mmoja wetu
aone ana jukumu kubwa la kulipa kipaumbele suala hili kwani ni kwa maendeleo
yetu na kwa mstakabali wa Taifa letu.
Ratiba ya wilaya itakayoanza mpaka
kuhitimisha, tutaitoa katika vyombo vya habari ili kila mtu kufahamu ratiba
yake na kujiandaa kwa usajili.
UNGUJA
WILAYA
|
TAREHE
|
WILAYA
|
TAREHE
|
WILAYA
|
TAREHE
|
Kusini
|
15–26/10/2012
|
Kati
|
29/10 – 09/11/2012
|
Magharibi
|
12 – 23/11/2012
|
Mjini
|
26/11 – 07/12/2012
|
Kask B
|
10 – 21/12/2012
|
Kask A
|
24/12/2012 – 04/01/2013
|
PEMBA
|
|||||
Mkoani
|
07 -18/01/2013
|
Micheweni
|
21/01 – 01/02/2013
|
Wete
|
04 – 15/02/2013
|
Chake Chake
|
18/02 – 01/03/2013
|
Vitambulisho hivi vitatolewa kwa makundi
makuu matatu, wananchi kwa ambao ni raia, wageni na wakimbizi. Hapa kwetu Zanzibar
tunaishi na wageni na hata wakimbizi. Rai yangu wote wajitokeze kujisajili kwa
kufuata taratibu na sheria za nchi, na
tusikubali kupindisha sheria kutoa kitambulisho cha uraia kwa wageni kwani sote
tunafahamu madhara yake, na umuhimu wa kila kundi kupewa kitambulisho chake kwa
kadiri ya stahiki zake.
Ndugu zangu tukifanya makosa katika
hili la kitambulisho tutajikuta nchi yetu kesho ikitawaliwa na wageni..tujifunze
kwa yaliyotokea kwa wenzetu, Tanzania yasitukute.
Ndugu Wanahabari,
Zipo faida nyingi
sana za kuwa na kitambulisho cha Taifa, kama ilivyo kwa kitambulisho cha
Mzanzibari mkaazi.
Wengi wetu tutakuwa tukijiuliza mfumo huu
wa Utambuzi na usajili wa watu utakuwa na faida gani kwetu kama Taifa na kama
wazanzibari?
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa
ikipata hasara nyingi kwa kushindwa kuwatambua watu wanaishio nchini kutokana
na kutokuwa na mfumo wa utambuzi na usajili wa watu Kitaifa. Baadhi ya hasara
hizo ni kama zifuatavyo:-
1.
Wananchi kuendelea
kuwa katika umasikini kwa kushindwa kupata mikopo katika benki na
taasisi za fedha. Faida ya zoezi hili, ni kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi. Aidha, baadhi ya benki zimekuwa
zinatoza riba kubwa kufidia hasara
wanayoipata kutokana na baadhi ya watu kutorudisha mikopo kwasababu hawatambuliki.
2.
Bodi
ya mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu imekuwa inapata matatizo na malalamiko
mengi kwa kushindwa kumtambua mwanafunzi yupi anastahili mkopo na
kwa kiasi gani. Aidha, urudishwaji wa mikopo hii umekuwa ni mgumu kwa kushindwa kuwapata wadaiwa mara baada ya kumaliza
vyuo na hivyo kuingizia hasara Serikali. Sasa kitambulisho cha Taifa
kitawezesha vijana wengi zaidi kupata mikopo ya elimu ya juu na hivyo kutoa
fursa kwa vijana wengi zaidi kuendelea kimasomo
3.
Kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu na hasa unaofanywa na
raia kutoka nchi jirani na wafungwa waliomaliza adhabu zao au kuachiwa
huru kwa msamaha wa Rais. Ni wazi kuwa udhibiti wao umekuwa mgumu kutokana na
kushindwa kuwatambua.
4.
Kuongezeka kwa mrundikano wa wafungwa katika magereza
mbalimbali kutokana na
kutokuwepo kwa udhibiti wa wafungwa wa kifungo cha nje.
5. Serikali imeendelea
kubeba mzigo mkubwa wa gharama wakati wa zoezi la kupiga kura. Kwakuwa na kitambulisho
cha Taifa, kutapunguza gharama kubwa za kuhuisha daftari la wapiga kura kila
inapohitajika
6. Serikali imekuwa
inapoteza fedha nyingi kila mwaka kwa kulipa watumishi hewa katika mfumo wa
mishahara ya watumishi wa Serikali. Sasa kwa kuwa na daftari lenye kumbukumbu
sahihi za watu, serikali itadhibiti upotevu wa fedha nyingi ambazo wamekuwa
wakilipwa watumishi hewa kwani hawatambuliki
7.
Pamoja na hayo, Serikali imekuwa inapata matatizo na
kuingia migogoro na wananchi wakati wa mazoezi ya kuwalipa fidia kutokana na kuchukua ardhi
au kubomolewa nyumba zao kwa
sababu ya kushindwa kumtambua mmiliki sahihi na anachokimiliki.
8.
Mfumo
huu pia utarahisisha na kuwawezesha vijana na watu wengi zaidi kuweza kumiliki
hati ya kusafiria (Passport) tofauti na hali ilivyo sasa ambayo inalazimu
mwombaji kuwa na vielelezo vingi kutokana na kutotambuana.
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanzisha Mfumo huu wa Vitambulisho vya
Taifa kwa sababu mbali mbali ikiwa ni pamoja na hizi zifuatazo:
1.
Kuweza
kuwatambua raia na wageni waishio Tanzania.
2.
Kusaidia kumtambua mhusika anapohitaji kupatiwa huduma
katika Taasisi mbalimbali
kama vile benki, taasisi za mikopo na huduma za afya.
3.
Kumtambua mtu pale
anapofanya uhalifu wa aina fulani. Jambo hili litasaidia sana
katika kupambana na uhalifu.
4.
Kuwatambua wakwepaji
wa kurejesha mikopo kutoka kwenye benki mbali
mbali nchini.
5.
Kuweka kumbukumbu za matukio ya uhalifu
katika daftari.
6.
Kumtambua mtu anapofanya
biashara au shughuli nyingine kwa kutumia majina
tofauti.
7.
Kuhakikisha kuwa mtu
anapata stahili zake za jamii. Kwa mfano, kupata malipo ya pensheni, haki za matibabu, haki za
kujiunga na masomo ikiwa ni pamoja na stahili zozote
ambazo raia wa Tanzania anastahili.
8.
Kusaidia katika
kuondoa watumishi hewa kwenye "payroll" ya Serikali.
9.
Kuimarisha utendaji
kazi Serikalini kwa kuwa na kumbukumbu sahihi za
watumishi na malipo ya stahili zao, hasa pale wanapostaafu.
10.
Kurahisisha zoezi la kuhesabu watu
(sensa).
11.
Kurahisisha
zoezi la kutengeneza daftari la wapiga kura.
12.
Kwakuwa
kitambulisho hiki kitakuwa cha teknolojia ya hali ya juu yaani (smart Card) na
kuweza kuhifadhi taarifa nyingi za mtu binafsi zikiwemo taarifa za kibailojia,
Kitambulisho cha Taifa kitasaidia kutambua watu panapotokea majanga kama vile
ajali n.k na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa haraka.
Ndugu
wanahabari,
Shughuli
hii ni mtambuka kwa maana ina mgusa kila mtu kwa nafasi yake, hivyo sitegemea
zoezi hili kuchukuliwa kuwa la kisiasa, kidini au kikabila, kwani lina linda
maslahi ya kila mmoja wetu. Huu sasa ni wakati wa kujenga umoja wa Kitaifa. Na
maamini Watanzania kwa hili tunaweza, na wazanzibari tutaonyesha mfano.
Rai kwa Wananchi wote
Napenda kuchukua fursa hii kuwaomba Wananchi
wote na wakazi wa Zanzibar mnaoishi
kihalali kujiandaa na kujitokeza katika
shughuli hii kwa kuhakikisha kuwa wale wote wenye umri wa miaka 18 na zaidi
wanaandaa na kutunza nyaraka zote muhimu zenye kumbukumbu zao binafsi ili
kurahisisha ushiriki wao katika zoezi hili kama watakavyoelekezwa.
Vyombo vya habari tunawaomba ushiriki
wenu wa karibu katika kuhakikisha kuwa
wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa wakati ili wasipoteze fursa hii muhimu
kwao ikiwa ni haki yao msingi kama raia.
Pia, napenda kutoa wito kwa Taasisi
zote za serikali wakiwemo wadau wote muhimu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya
Taifa (NIDA) ambao ni RGO, ZAN-ID,
UHAMIAJI na TAMISEMI tushirikiane kwa pamoja ili wananchi wote na wageni
wanaoshi nchini kihalali kusajiliwa.
Mwisho
NIDA inawahakikishia wananchi wote, usiri mkubwa wa taarifa zitakazotolewa na
utunzaji wa taarifa hizo muhimu wakati wote wa zoezi hili, mpaka kupatokana kwa
Vitambulisho.
Asanteni sana
kunisikiliza.
Vuai Mussa Suleiman,
Mkurugenzi
Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa
Zanzibar.
03 / 10 / 2012
No comments:
Post a Comment