Nkyandwale
Franco, Sumbawanga
KIKUNDI
cha wanawake wajasiriamali cha UAMSHO
kilichopo katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, kinachojumuisha wanawake
wafanyakazi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa na wale taasisi binafsi kimeshauriwa
kufanya biashara zao kitaalam kwa lengo
la kuongeza zaidi.
Ushauri
huo umetolewa na mmoja wa wanakikundi hao ambaye pia ni Mkurugenzi wa Chuo Kikuu Huria tawi la Rukwa, Dk. Elna
Lyamuya mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Stella Manyanya kuitisha
kikao cha pamoja cha watendaji wake wa kike
kilicholenga kuunda kikundi hicho.
Dk.
Lyamuya alisema ili wanawake hao waweze kujikomboa na kufanya biashara zao
kuendana na kasi ya mabadiliko ya kitenolojia ni lazima wajikite katika elimu
itakayowasaidia kunufaika na biashara wanazozifanya zikiwemo zile za usindikaji
vyakula,uuzaji wa nafaka pamoja na zile ufugaji wa kuku na ng’ombe wa kisasa.
Wanawake
hao pia wameshauriwa kufanya mchakato wa bidhaa zao kuanzia kuzalisha hadi kufikia
hatua za uuzaji kwa lengo la kuwafanya
wao waweze kufahamika kibiashara bila kusahau kuboresha ubora wa bidhaa zao.
Awali
katika kikao hicho Mkuu huyo wa Mkoa alisema lengo la kuunda umoja huo
unaolenga kuelimisha wanawake wengine kuondokana na dhana tegemezi ni kuwasaidia wanachama katika masuala ya elimu.
Mara
baada ya kikao hicho, wanawake hao waligawiwa kanga zilizotolewa na Mkuu wa
mkoa kama
kumbukumbu ya uanzishili wa chama hicho.
No comments:
Post a Comment