Wauzaji wa tiketi mikononi wakimzonga mmoja wa abiria kwa kila mmoja akitaka kumuuzia tiketi katika maeneo ya bandari ya malindi Zanzibar.
Serekali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Taasisi husika na Usafiri wa Majini Zanzibar kupiga marufuku uuzaji wa tiketi mikononi, lakini bado kuna baadhi ya Wananchi hutumia njia hiyo kuuza tiketi bila kujali taarifa hiyo ya serekali kuhusu agizo lake.Sheria hiyo imeweka kujuwa wasafiri wanaosafiri wakati wa safari zao ikiwa ni tahadhari na madhara yakitokea ili kujuwa majina ya abiria waliosafiri na chombo hicho.
Lakini bado sijui Wananchi hawaelewi usalama wao na mali zao wakati mwa kutokea ajali ili kutambuliwa kwa urahisi na kupata haki zao wanazotakiwa kupata wakati wa janga likitokea.kujuwa idadi kamili ya abiria waliosafiri na chombo hicho.
Taasisi husika na vyombo vya Usalama inabidi kulichukulia tatizo hili kuwa la Taifa ili kila mtu kutambua sheria za Usafiri wa Baharini na kununua tiketi katika Ofisi husika ili kupata hesabu kamili ya abiria.
Wizara ya Mawasiliano na Miundombinu ilitowa agizo kupitia Mamlaka ya Usafi wa Baharini Zanzibar, kila Ofisi zinazotowa huduma wa Usafiri wa baharini wasiuze tiketi bila ya abiria kuwa na kitambulisho cha kumtambulisha ili kuweza kupata tiketi kwa safiri ya Dar-es-Salaam au Pemba.
Jamani chondechonde tusidharau sheria hii ni kwa faida yetu na familia zetu katika kufanya safari, sio kila siku kuitupia lawama Serekali haina utaratibu wa kusimamia za baharini wakati wa kutokea ajali na kusema abiria walikuwa zaidi ya uwezo wa chombo husika, ilivyotokea wakati wa kuzama kwa meli ya Mv Spice kila mtu amesema abiria walikuwa zaidi ya elfu tatu, kutokana na kukosa orodha kamili wa abiria wanaokata tiketi sehemu husika.
Kwa hiyo tufuate sheria hii ili kutokurudia makosa ya nyuma na kupata hesabu kamili ya abiria wanaosafiri katika vyombo vinavyofanya safari za kati ya Pemba na Unguja na Unguja na Dar-es- Salaam.
Hii ni faida yetu na si faida ya mtoa huduma ya usafiri au kwa mtu mwengine yoyote yule, tuache tabia hii na kufuata sheria za kutowa huduma kwa faida ya taifa.
No comments:
Post a Comment