Habari za Punde

Dk Shein kufungua mkutano wa 34 wa AAPAM kesho

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein kesho anatarajiwa kufunguwa Mkutano wa 34 wa Juimuia ya kiafrika ya Utumishi wa Umma na Uongozi(AAPAM) huko Zanzibar Beach Resort nje kidogo wa Mji wa Zanzibar.
Kwa mujibu wa Ratiba iliotolewa na Jumuia hiyo imeonesha kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi DKT Abdulhamid Yahya Mzee atatowa maelezo juu ya Mkutano huo.
Baadae Rais wa AAPAM Abdon Agaw Jok Nhial nae atatowa maelezo juu ya Mkutano huo kwa upande wa Jumuia hiyo ambapo pia Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania Celina Kombani atatowa Maelezo na baadae kumkaribisha Mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ambae atahutubia Mkutano huo.
Wajumbe kadhaa wa Mkutano huo tayari wameshawasili Zanzibar akiwamo Katibu Mkuu wa AAPAM .
Jumla ya Wajumbe 500 wanatarajiwa kushiriki katika Mkutano huo ambapo mwaka jana Mkutano kama huo ulifanyika Nchini Malawi.
Mbali na Mkutano huo Wajumbe hao pia watapata fursa yakutembelea sehemu mbali mbali za vivutio vya Utalii viliopo Zanzibar pamoja na kutembelea Mji Mkonge na sehemu za Historia.
Mkutano Huo wa AAPAM wa siku tano unatarajiwa kumalizika tarehe 16/11/2012

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.