Habari za Punde

KCB Zanzibar Yatowa Elimu kwa Wateja Wake.


Mkuu wa Masoko na Uhusiano - KCB Bank, Imelda Gerid,akitowa utangulizi  katika mkutano wa kutowa elimu kwa Wateja wa Bank ya KCB Tawi la Zanzibar, katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace  Malindi Zanzibar.
 Mwakilishi wa Kitengo cha Mauzo kwa Wateja Binafsi -KCB Bank,Fredirick Lyimo, akitowa elimu kwa huduma za Wateja zinazotolewa na benki hiyo kwa wateja wake katika matawi yao, akizungumza wakati wa mafunzo kwa wateja wa tawi la Zanzibar katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar. 

  Wateja wa Banki ya KBC  Tawi la Zanzibar wakifuatilia mada zinazotolewa na Maofisa wa benki ya KBC .




Maofisa wa Bank ya KCB wakisikiliza michango ya washiriki wa Semina ya Elimu kwa Wateja wa Benki ya KCB, inayofanyika katika hoteli ya Grand Palace Malindi.

Mfanyabishara wa Zanzibar akichangia katika semina hiyo 

Mfanyabiasha wa Duka la Pamba land akihoji utaratibu wa jinsi ya kupata mkopo katika benki ya KCBna njia za kupata mkopo.na kutowa mfano yeye imemchukuwa muda kupata mkopo huo na kuingia hasara.

Mfanyabiashara Mohammed Masoud, akizungumzia kuhusu kiasi cha kupata mkopo kwa mteja wa benki hiyo,
Mdau wa Benki ya KCB Zanzibar Dulla akiuliza suali katika semina hiyo ya Wafanyabiashara Zanzibar kuwawezesha kiuchumi katika biashara zao.

Mfanyabiashara wa  Mohammed Ayoub akichangia katika mkutano huo wa Elimu ya iliotolewa na Benki ya KCB Tawi la Zanzibar 
Muwezeshaji  wa Benki ya KCB Fredirick Lyimo, akinukuu  maswala ya Washiriki wa Semina ya Siku moja ilioandaliwa na Benki ya KCB kwa Wateja wake.
Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Zanzibar akifafanua jambo katika semina ya Wafanyabiashara iliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Grand Palace Malindi Zanzibar.
Meneja Mikopo wa KCB Tawi la Zanzibar Said akijibu  maswala yalioulizwa na washiriki wa semina hiyo iliowashirikisha Wafanyabiashara na Wajasiriamali jinsi ya kupata huduma  za mikopo katika benki hiyo. 


Na Mohammed Mhina, Zanzibar
Benki ya KCB nchini imeanza kutoa mafunzo kwa wajasiliamali wadogo na wa kati ili kuwawezesha kukuza miradi na mitaji yao kiuchumi.
Wakizungumza wakati wa mafunzo hayo, Wakufunzi wa Benki hiyo wamesema kuwa pamoja na mambo mengine nia ya mafunzo hayo ni kuongeza uwelewa wa namna ya kuendesha biashara ndogondogo kwa wajasiliamali na jinsi ya kutunza fedha benki.
Wakati wa mafunzo hayo, Bw. Fredrick Lyimo na Bw. Francis Mandala, wamesema kuwa benki hiyo imeweza kuboresha huduma zake ili kuwezesha wateja wake kunufaika na ujasiliamali wao.

Wamesema kuwa pamoja na kutoa elimu hiyo kwa wajasiliamali, KCB Bank ambayo ina matawi katika nchi zote tano za Afrika ya Mashariki, pia hutoa misaada mbalimbali ikiwemo ya Vifaa vya Afya, Elimu na huduma nyingine za kijamii.
Washiriki hao wameelimishwa jinsi ya kuweza kuomba na kupatiwa mikopo pamoja na kufundishwa jinsi ya kuitumia mikopo wanayoipata.
Akitoa elimu juu ya miashara na mitaji, mmoja ya wakufunzi Bw. Peace Lumelezi, amesema kuna haja ya kila mfanyabiashara kutofautisha biashara yake naya mwingine ili kupata faida.
Amesema kuwa hata kama biashara ya mfanyabiashara mmoja inafanana naya mwingine katika eneo moja, lakini ni lazima kufanyabiashara makini atofautishe biashara yake hata kwa lugha kwani wateja wanahitaji huduma bora.
Amewashauri pia wafanyabiashara kutokwepa kodi za Serikali na kujiwekea bima ili kuepuka ajali na hasara za majanga ya moto ama wizi.
Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo, wameelezea changamoto mbalimbali zinazowakuta na kusema baadhi ya waomba mikopo wamekuwa wakitoa taarifa za uongo katika mabenki ili mradi waweze kupatiwa mikopo jambo ambalo halijengi uaminifu kwa taasisi za fedha.
Pamoja na kuelezea kunufaika na mafunzo hayo, washiriki hao pia wameiomba benki ya KCB hapa nchi kuangalia uwezekano wa kuongeza matawi zaidi ya kenki hiyo pamoja na kuongeza idadi za mashine za kutolea fedha yaani ATM karibu na maeneo yenye wananchi wengi.
Wamesema kwa ulimwengu wa sasa hakuna mtu anayependa kutembea na fedha nyingi mfukoni kwa kutoka eneo moja hadi jingine kwa kuhofia kuporwa ama kuibwa kwa fedha zake.
Wamesema kama kutakuwa na matawi mengi ya benki ni rahisi kwa wajasiliamali kufanya biashara zao na kuweka fedha zao benki lakini wakazichukua hata kwa kupitia katika mashine za ATM pale wanapozihitaji kwa matumizi ya kawaida ama ya kibiashara. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.