Habari za Punde

Rais wa Zanzibar Dk. Shein, Atowa Salamu za Pongezi Viongozi wa Nchi za Falma za Kiarabu UAE.

STATE HOUSE ZANZIBAROFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 30.11.2012

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewatumia salamu za pongezi viongozi wa nchi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), kwa kutumiza miaka 41 ya Taifa hilo.

Katika salamu hizo za pongezi Dk. Shein amemtumia salamu Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu ambaye pia ni kiongozi wa Abu Dhabi Sheikh Khalifa Bin Zayed Al Nahyan, kiongozi wa Ras Al Khaimah Sheikh Saud Bin Saqr Al Qasimi, Kiongozi wa Sharja Sheikh Dk. Sultan Bin Mohammed Al Qasimi na kiongozi wa Dubai Sheikh General Mohamed Bin Rashid Al-Maktoum.

Katika salamu hizo za pongezi Dk. Shein alichukua fursa hiyo kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar kutoa pongezi kwa kutimiza miaka 41 ya nchi hizo za Umoja wa Falme za Kirabu na kuwapongeza viongozi hao pamoja na wananchi wao wote wanaowaongoza.

Salamu hizo zilitoa pongezi kwa mafanikio makubwa yaliopatikana katika nchi za Umoja huo kutokana na uongozi mzuri katika kuzipelekea maendeleo nchi zao.

“Tuanajivunia uongozi imara wan chi za Umoja wa Falme za Kiarabu na sisi watu wa Zanzibar tumevutiwa sana na maendeleo yaliofikiwa katika nchi hizo na tunatoa pongezi za pekee”,zieleza salamu hizo alizotuma Dk. Shein.

Aidha, salamu hizo ziliwaombea dua kwa Mwenyezi Mungu kuwapa umri mrefu na afya njema katika kuziendeleza nchi zao viongozi wote wa UAE.

Pamoja na hayo, salamu hizo zilieleza kuwa Zanzibar itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake kwa nchi hizo pamoja na wananchi wake.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.