Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk, akizungumza na Viongozi wa Vilabu vya Michezo Zanzibar, kujuwa utaratibu wa vilabu hivyo katika kukuza michezo yao ndani ya klabu zao. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Mnazi Mmoja.
Rais wa Klabu ya Michezo ya Watu wenye Ulemavu wa Kutokusikia (Viziwi) Zanzibar Juma Abrahaman, akitowa maelezo ya klabu yake kwa waziri,wakati wa kikao hicho kilichowajumuisha makatibu wa vilabu.
Kiongozi wa Vilabu vya Karata Zanzibar, akielezea matatizo inayokabili vilabu vya karata kwa uongozi.
Kiongozi wa mchezo wa bao akichangia katika mkutano huo.
Kiongozi wa Mchezo wa Gofu Zanzibar akitowa maelezo yake kwa Waziri wa Michezo.
Mkalimani wa lugha za watu wasiosikia akitowa ishara ya vitendo kwa maneno yanayozungumza katika mkutano huo.
No comments:
Post a Comment