Baraza la Wawakilishi limechukua hatua mbali mbali katika kuhakikisha kunakuwa na ushiriki mkubwa zaidi wa wananchi hasa katika mchakato wa utungaji wa Sheria za nchi.
Miongoni mwa hatua hizo ni kusomwa kwa miswada kwa mara ya kwanza katika mkutano mmoja na kujadiliwa na kupitishwa katika Mkutano wa Baraza unaofuatia ili kutoa fursa ya kutosha kwa wananchi kushiriki katika kutoa maoni yao.
Kufuatia mabadiliko ya Kanuni za Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuelekeza miswada ya Sheria kusomwa kwa mara tatu, Kanuni inaelekeza baada ya miswada hiyo kusomwa mara ya kwanza itangazwe kwa wananchi ili waifahamu miswada hiyo na waweze kushiriki kutoa maoni yao mbali mbali.
Katika Mkutano wa Kumi wa Baraza la Nane la Wawakilishi miswada ifuatayo itajadiliwa.
1. Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Usafiri wa Baharini Nam. 5 ya mwaka 2006
2. Msawada wa Sheria ya Kuanzisha Shirika la Utangazaji Zanzibar, kazi, majukumu na utawala wake pamoja na mabo mengine yanayohusiana na hayo
3. Mswada wa Sheria ya kuanzisha Shirika la Meli Zanzibar, kazi, uwezo na mambo mengine yanayohusiana na hayo
4. Mswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ruzuku kwa Vyama vya Siasa Nam. 6 ya mwaka 1997 na mambo mengine yanayohusiana na hayo
Ili kupata michango mbali mbali wananchi wanakaribishwa kutoa maoni kuhusia na miswada
hiyo. Maoni yawasilishwe kwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi kwa njia ya maandishi, si zaidi ya tarehe
4 Januari, 2013.
Aidha, nakala za miswada hiyo zinapatikana katika Afisi ya Katibu wa Baraza la Wawakilishi na
hivyo kila mwananchi atakayependa, anaweza kuomba kupatiwa nakala hizo.
Maoni yatumwe kupitia anauni zifuatazo:-
1. Sanduku la Posta (S.L.P. 902, Zanzibar)
2. Barua pepe (zahore@zanlink.co au
3. Yaletwe Afisi ya Baraza iliyopo Chukwani
Imetolewa na:
…………………………………
Amour M. Amour
Kny: KATIBU,
BARAZA LA WAWAKILISHI,
ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment