Habari za Punde

Dk Shein afanya uteuzi wa wenyeviti wa Bodi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein ,amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbali mbali katika Wizara ya Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati,Zanzibar.
Dkt Shein amemteuwa Ashrak Mahmoud Hamid kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili,Wasanifu,Wahandisi na Wakadiriaji Ujenzi,Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi,Dkt Abdulhamid Yahya Mzee amesema kuwa uteuzi huo wa Rais ameufanya kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 4(1)(a) cha Sheria ya Bodi ya Wakandarasi Namba 5 ya mwaka 2008.
Aidha Dkt Shein amemteuwa Rama Keis Mgeni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakandarasi, Zanzibar.
Rais amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 5(1)(a) cha Sheria ya Bodi ya Wakandarasi Namba 6 ya mwaka 2008.
Uteuzi huo umeanza jana tarehe 12/12/2012.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.