Habari za Punde

Semina - Athari za uvuvi haramu na udhibiti wake yafanyika Zanzibar

 Baadhi ya Wajumbe walioshiriki katika Semina ya Uwelewa juu ya Athari za Uvuvi Haramu na Udhibiti wake unaotokana na Sheria mpya ya Uvuvi namba 7 ya mwaka 2010.huko katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje ya Mjiwa Zanzibar.
 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdillahi Jihad Hassan akifungua Semina kuhusu Uwelewa juu ya Athari za Uvuvi Haramu na Udhibiti wake unaotokana na Sheria mpya ya Uvuvi namba 7 ya mwaka 2010.huko katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
 Mkurugenzi wa wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Mussa Aboud Jumbe akionyesha Nyavu za kukokota ambazo ni hatari kwa kuuwa matumbawe na mazalio ya Samaki katika Semina kuhusu Uwelewa juu ya Athari za Uvuvi Haramu na Udhibiti wake unaotokana na Sheria mpya ya Uvuvi namba 7 ya mwaka 2010.huko katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
 Mkurugenzi wa wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Mussa Aboud Jumbe katikati akionyesha Dema lililotengenezwa kwa Waya ambalo ni baya kwa kuharibu Matumbawe na kuvuwa samaki wachanga katika Semina kuhusu Uwelewa juu ya Athari za Uvuvi Haramu na Udhibiti wake unaotokana na Sheria mpya ya Uvuvi namba 7 ya mwaka 2010.huko katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi Mussa Aboud Jumbe akionyesha Kikopo ambacho hutumika kwa Kuvulia Pweza na kinacho kubalika kisheria katika Semina kuhusu Uwelewa juu ya Athari za Uvuvi Haramu na Udhibiti wake unaotokana na Sheria mpya ya Uvuvi namba 7 ya mwaka 2010.huko katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mbweni nje ya Mji wa Zanzibar.
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI-MAELEZO ZANZIBAR.20/12/2012

2 comments:

  1. Hapana uvuvi hapa, kazi kuharibu pesa tu kwa vikao na semina zisizokwisha.

    Hivi inakuwaje Ziwa viktoria lizalishe samaki wa kutosha kulisha wakaazi 2,700,000 wa mwanza na kusafirisha nje minofu, halafu Z'bar ishindwe hata kutosheleza watu wake..kula samaki hapa imekua 'anasa' hii wizara bora hata ifutwe..imeshindwa kazi kabisa!

    ReplyDelete
  2. Tatizo kuwa ni Uongozi wa Idara ya Uvuvi kuanzia Mkurugenzi wa Uvuvi hadi chini wengi wao ni wabadhirifu kazi kujitajirisha. Pili, Maofisa wote wananalamika kuwa hawana sauti ya kusema chochote kwani mambo yote yanaamuliwa kwa ubabe na Mkurugenzi na yeye hana elimu ya Uvuvi ila ana elimu ya mazingira ya bahari nchini India hilo ndio sababu kubwa ya Idara ya Uvuvi kutoweza kwenda mbele.

    Kama hakujafanywa mabadiliko ya Uongozi kwenye Idara hiyo basi maendeleo itakuwa ndoto

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.