
Mfungaji wa penalti ya mwisho na ya ushindi ya Zanzibar, Abdallah Othman akikimbia kushangiria baada ya kumaliza mechi ya Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge dhidi ya Burundi kwenye Uwanja wa Lugogo mjini Kampala, Uganda, Zanzibar ilishinda kwa penalti 6-5 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Ndikumana chini, shughuli ya Issa Othman Ally kushoto

Aggrey Moris akimdhibiti mshambuliaji wa Burundi

Suleiman Kassim Selembe kulia anakokota ngoma

Abdulaghan Gullam akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Burundi

Aggrey Morris anapanda kusaidia mashambulizi baada ya kuokoa

Selembe anapasua katikati ya watu

Issa Othman Ally anaondoka na mpira mbele ya wachezaji wa Burundi

Jaku Juma akipambana na beki wa Burundi

Ndikumana akijuta baada ya kukosa penalti

Balozi wa Tanzania nchini Uganda, kulia akimpongeza kocha wa Zanzibar Heroes, Salum Bausi

Wachezaji wa Zanzibar wakimpongeza Abdallah Othman baada ya kufunga penelti iliyowauwa warundi

Wachezaji wa Zanzibar na baadhi ya viongozi wakimpongeza Abdallah Othman katikati aliyesujudu
Picha zote kwa hisani ya Bin Zubeiry, Kampala
No comments:
Post a Comment