Habari za Punde

Balozi Seif afungua skuli mpya ya sekondari ya Mikindani

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanziubar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia moja ya daraza la Skuli ya Sekondari Mikindani Dole wilaya ya Magharibi mara baada ya kuiozindua Skuli hiyo
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiizindua rasmi Skuli Mpya ya Sekondari ya Mikindani Dole Wilaya ya Magharibi ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar
Balozi Seif akiangalia Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Mikindani Dole ambayop imekamilika mahitaji ya vifaa kwa wanafunzi wa skuli hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpongeza Mwakilishi wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Uchumi na Elimu Bwana Nobuyuki Tanaka ambaye Taasisi yake imegharamia ujenzi wa Skuli ya Sekondari ya Mikindani Dole.
 
Na Othman Khamis Ame
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliifungua rasmi Skuli mpya ya Sekondari ya Mikindani iliyopo Dole Wilaya ya Magharibi.
Skuli hiyo mpya inatarajiwa kuwaunganisha wanafunzi wa Skuli za Vijiji vya Dole, Kianga, Langoni, Mwenge na Kijichi ikiwa na uwezo wa kuchukuwa Wanafunzi 320.
Zaidi ya shilingi Bilioni Moja nukta Moja zilizotolewa mkopo na Benki ya Dunia zimetumika katika ujenzi wa Skuli hiyo yenye majengo manne,Maabara, Maktaba ikiwa na wanafunzi 160 na walimu 16.

Akizungumza na Walimu wanafuni na wananachi wa maeneo hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema Serikali itaendelea kutafuta Walimu wenye sifa sambamba na Vifaa ili kujenga Taifa bora lenye wataalamu wa kutosha.
Balozi Seif alifahamisha kwamba Taifa bado lina upungufu wa wataalamu, hivyo wanafunzi nchini wana nafasi ya kuzitumia fursa zilizopo ambazo tayari serikali imeshawajengea mazingira bora ya kielimu.
Mapema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Abdulla Mzee alisema mradi wa uimarishaji wa elimu ya lazima Zanzibar chini ya Mkopo wa Benki ya Dunia umekusudia kujenga skuli 19 Zanzibar ambapo kila Wilaya itakuwa na Skuli mbili za aina hiyo.
Nd. Abdulla alisema mradi huo unaotarajwa kugharimu jumla ya dola za Kimarekani Milioni 42,000,000 sawa na Shilingi Bilioni 62 za Kitanzania unahusisha pia uchapishaji wa Vitabu.
Naye kwa upande wake Mwakilishi wa shirika la Fedha Duniani {WB } katika masuala ya Elimu na Uchumi Bwana Nobuyuki Tanaka ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua zake za kuimarisha sekta ya elimu.
Bwana Tanaka alisema hatua hiyo itaiwezesha Zanzibar kwenda sambamba na mabadiliko ya haraka ya sayansi na teknolojia ambayo tayari yanakamilika katika mfumo wa Digital.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.