Habari za Punde

Balozi Seif atoa maoni yake katiba mpya

 Mwenyekiti wa Kamati ya kukusanya Maoni ya Katiba Mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Jaji Joseph Sinde Warioba na Timu yake akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi walipofika Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kupokea Maoni yake.
Pembeni kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dr. Salim Ahmed Salim na pembeni Kulia ni Mjumbe wa Kamati hiyo Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania Mh. Agostino Ramadhan.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoa Maoni yake binafsi kuhusu Mfumo wa Muundo wa Katiba Mpya ya Muungano wa Tanzania mbele ya Kamati ya kukusanya maoni hayo inayoongozwa na Jaji Joseph Sinde Warioba.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Kukusanya Maoni kuhusu Katiba Mpya ya Tanzania mbele ya mlango wa Ofisi yake vuga Mjini Zanzibar.
Kulia ya Balozi Seif ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dr. Salim Ahmed Salim, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jaji Joseph Sinde Warioba na Nd. Abou Bakar. Na Kushoto ya Balozi ni Jaji Maria Koashonda.
Picha no Hassan Issa wa – OMPR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.