Habari za Punde

Kamati ya Mandalizi ya Michuano yakusherehekea miaka 36 ya CCM Wilaya ya Mjini.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Michuano ya kuadhimisha miaka 36 ya CCM Wilaya ya Mjini Nassor Salim Jazira, akizinduwa machuano hiyo kwa kutoa ratiba ya mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika katika uwanja wa Mao.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Michuano ya kuadhimisha miaka 36 ya CCM Wilaya ya Mjini Nassor Salim Jazira, akimkabidhi Katibu wa Jimbo la Kikwajuni Kassim Ali, kwa niaba ya majimbo yote makabidhiano hayo yamefanyika katika Tawi la CCM Kilimani.
 Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mahmoud Mohammed Mussa, akitowa shukrani kwa niaba ya Majimbo yote ya Wilaya ya Mjini na kutowa ahadi ya kutowa zawadi kwa Washiriki wa michuano hiyo inayoshirikisha Majimbo ya Kikwajuni, Rahaleo, Jangombe Mji Mkongwe na Kwahani. 
 Waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi wa maandalizi ya michuano ya kusherehekea miaka 36 ya CCM, itakayoshirikisha Majimbo matano ya Wilaya ya Mjini.uzinduzi huo umefanyika katika Tawi la CCM Kilimani. 
Viongozi wa  timu za Majimbo ya Wilaya ya Mjini wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Michuano ya Kusherehekea miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi akizindua na kukabidhi Jezi kwa ajili ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.