MISWADA minne ya Sheria
inatarajiwa kuwasilishwa na kujadiliwa katika kikao cha Baraza la Wawakilishi
kinachotarajiwa kuanza leo huko Chukwani nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Katibu wa Baraza la
Wawakilishi Zanzibar, Yahya Khamis Hamad, alisema hayo jana katika mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika ofisi za Baraza hilo.
Aliitaja miswada
itakayowasilishwa kuwa ni pamoja na mswada wa sheria ya marekebisho ya sheria
ya usafiri wa baharini nambari 5 ya mwaka 2006.
Mswada mwengine ni wa
sheria ya kuanzisha Shirika la Utangazaji Zanzibar, Kazi, Majukumu na Utawala
wake pamoja na mambo mengine yanayohusiana na hayo.
Katibu huyo wa Baraza
alisema pamoja na mambo mengine lakini pia kikao hicho kitapokea mswada wa
Sheria ya kunzisha Shirika la Meli Zanzibar, Kazi, Uwezo na mambo mengine
yanayohusiana na hayo.
Aidha mswada mwengine ni
pamoja na sheria ya marekebisho ya Sheria ya Marekebisho ya sheria ruzuku kwa
vyama vya siasa nambari 6 ya mwaka 1997 na mambo ynayohusiana na hayo.
Sambamba na hilo lakini pia
Baraza hilo litapokea ripoti ya kamati Teule ya kuchunguza utendaji wa Shirika
la Umeme Zanzibar.
Kikao hicho kinatarajiwa
kuwa cha wiki mbili pia kitaweza kuwa na maswali na majibu 117 ambayo
yataulizwa na wajumbe wa Baraza hilo na kujibiwa.
No comments:
Post a Comment