Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikagua kikosi cha Simba kilichopambana na timu ya Jamhuri katika ufunguzi wa kombe la Mapinduzi “Mapinduzi Cup 2013” uwanja wa Amaan. Katika pambano hilo Simba ilianza vizuri kwa kuifunga Jamhuri (4-2).
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad akisalimiana na Wachezaji wa Timu ya Jamuhuri wakati wa mchezo wa Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi zinazofanyika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika jukwaa akifuatilia mchezo wa Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup, kati ya mchezo Simba na Jamuhuri uliofanyika uwanja wa Amaan, timu ya Simba imeshinda 4-2, kushoto Rais wa ZFA Taifa Amani Ibrahim Makungu na kulia Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk .
Mchezaji wa timu ya Jamuhuri Msafiri Leornad akimpita beki wa timu ya Simba.
Kocha mpya wa Simba kutoka Nchini Ufaransa akifuatilia mchezo wa timu yake na wakati ikicheza na timu ya Jamuhuri akiwa na Viongozi wa Simba Zanzibar Abdull Mshangama wakiwa katika jukwaa la VIP.
Kocha mpya wa timu ya Simba akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumalizika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi kati ya Simba na Jamuhuri timu ya Simba imeshinda 4--2.
No comments:
Post a Comment