Habari za Punde

Mke wa Rais wa Zanzibar Akabidhi Vifaa Hospitali ya Kivunge na Vikundi vya Wanawake.

 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni akimkabidhi  Viti vya Wagonjwa kwa ajili ya kutolea huduwa katika hospitali ya Kivunge, akipookea vifaa hivyo Mkurugenzi Tiba Dr. Salhia Ali Muhsini, makabidhiano hayo yamefanyika katika Hospitali ya Kivunge Unguja Mkoa wa Kaskazini

 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni akiangalia baadhi ya mashuka kabla ya kumkabidhi  Mkurugenzi Tiba Dr. Salhia Ali Muhsini, makabidhiano hayo yamefanyika katika Hospitali ya Kivunge Unguja Mkoa wa Kaskazini 
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni akizungumza na wanachama wa Nungwi Saccos hapo katika Tawi la CCM Nungwi. kushoto yake ni Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi ,na Kushoto yake ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Bibi Salama Aboud Talib.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni akijiandaa kukabidhi mchango wa shilingi 2,000,000/- kwa Katibu wa Nungwi Saccos Bibi Siti Ali Makame kutekeleza ahadi ya Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete.
 Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni akikabidhi mchango wa shilingi 2,000,000/- kwa kikundi cha Nungwi Saccos  kutekeleza ahadi ya Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mama Slma Kikwete aliyoitoa mwezi Mei mwaka 2010.
Akina mama wa Ushirika wa Nungwi Saccos wakishangiria mchango wa shilingi milioni 2,000,000/- zilizotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni ambazo ziliahidiwa na Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete wakati akiizindua Nungwi Saccos Mwaka 2010

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.