JUMUIYA ya Mchezo wa GOJU-RYU
KARATE Zanzibar
hatimai yapata viongozi wake katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika katika ukumbi wa
Judokan Amaan. Jumuiya hiyo kwa muda mrefu ilikuwa na Uongozi wa muda.
Kwa mujibu wa Msimamizi wa
Uchaguzi huo amesema uchaguzi huo umefanyika kwa taratibu zote za Katiba ya
Jumuiya hiyo na kupata Viongozi wake kwa kupitia uchaguzi huo, ambao ulikuwa na
mvutano kwa panda za Nafasi za Mshika Fedha na Katibu Mkuu.
Uchaguzi huo umesimamiwa na Kaimu
Katibu Mkuu wa Chama cha Karate Taifa
Zanzibar, Haji Hassan Hussein, amesema uchaguzi huo umefanyika kwa haki za
taratibu zote za Katiba ya Jumuiya hiyo na kupata Viongozi halali watakaogozi
Jumuiya hiyo kwa muda wa miaka minne.
zilikuwa
Amesema katika nafasi
zilizongombewa katika jumuiya hiyo ni nafasi ya Mwenyekiti ambayo haikuwa na mpizani ilikuwa na mgombea
Hamad Suleiman, ambaye ameshinda kwa kura 15,na kura mbili zimeharibika, kwa
nafasi ya Makamu Mwenyekiti Unguja ameshinda Salum Amuor Nassor kwa kura 16,na
kwa Pemba ameshinda Ridhiwan Mohammed Salum kwa kura 14.
Kwa nafasi za Katibu Mkuu na Mshika fedha zilikuwa na upinzani kwa
wagombea wake kwa baadhi ya wagombea kututimiza masharti ya Katiba ya Jumuiya
hiyo.amesema nafasi hiyo ya Katibu Mkuu imechukuliwa na Haji Kombo Faki kwa kura
13, na mpizani wake Said Seif Abdalla amepata kura 3.Msaidizi Katibu Mkuu
Unguja imechukuliwa na Mohammed Nour kwa kura 15 na kwa Pemba imechuliwa na
Khalfan Suleiman kwa kura 16.
Amesema kwa nafasi za Mshika
fedha wagombea wake wamechuana vikali na kuibuka mshindi kwa kura chache na
kuibuka mshindi Yusuf Abrahaman Najim kwa kura 8 dhidi ya mpizani wake Hamadi
Juma Said amepata kura 7, na kwa upande wa Mshika Fedha Msaidizi Unguja
imechukuliwa na Ramadhani Rashid
Mohammed kwa kura 15 na kwa Pemba imeshikiliwa na Abdalla Omar Ali.
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha
Karate Taifa Zanzibar Haji Hassan Hussein amewashukuru washiriki wa uchaguzi
huo na kuwapongeza Wajumbe wate wa Mkutano Mkuun wa Jumuiya hiyo kwa utulivu
wao wakati wote wa uchaguzi hati tamati ya shughuli hiyo na kuwapata washindi.
Amewataka washindi wa uchaguzi
huo kufanya kazi zao kwa umoja ili kuivusha Jumuiya hiyo katika mashindano yake
ya Ndani na Njee ya Zanzibar wakati wa ushiriki wake na kukipa mafanikio katika
kipindi chao cha uongozi.
No comments:
Post a Comment