Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Hussien Ibrahim Makungu (BHAA) ameongeza basi jengine kwa
ajili ya kutowa huduma ya Usafiri kwa Wanafunzi wa Jimbo lake
kuondosha kero ya usafiri kwa
Wanafunzi inayowakabili wanafunzi katika Visiwa vya Zanzibar.
Amesema ameamua kuongeza basi jengine baada ya kuona basi lililokuweko halitoshi kwa wanafunzi hao.
Hayo ameyaeleza leo wakati akiwa katika kituo cha daladala
darajani wakati akikabidhi basi hilo
kwa wanafunzi wanaotoka skuli mchana na kuanza kutowa huduma hiyo na kufanya
idadi ya mabasi kuwa mawili yakitowa
huduma hiyo kuanzia leo.
Amesema hayo aliyokuwa amewaahidi Wananchi wa Jimbo lake wakati
wa uchaguzi anayatimiza na ikiwemo kukimalizia ujenzi wake kituo cha afya
Mwanyanya na kuyaimarisha matawi ya CCM katika jimbo hilo kwa kuyawekea umeme na
kuwaletea maendeleo wananchi wa jimbo la bububu na kupiga hatua mbele katika
maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Nae Mwenyekiti wa
CCM wa Mkoa wa Magharibi Yussuf
Mohammed amempongeza Bhaa kwa jitihada
zake na utendaji wake uliochukuwa muda mfupi kutimiza ahadi alizozitowa wakati
wa kampeni yake katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, na alipoingia madarakani
ametekeleza ahadi zake kwa kiasi kikubwa
kwa kutowa vifaa mbalimbali katika jimbo lake na kumtaka kuendelea na
juhudi zake kuliletea jimbo hilo maendelea zaidi.
Tujenge wivu wa kimaendeleo na tusijenge uchoyo na
ubinafsi ,alisema Yussuf na kuwasihi viongozi hao.
Amewataka Wananchi vifaa hivyo wavitunze kama
inavyotakiwa pia amesisitiza kudumisha umoja na mshikamano katika jimbo lao
ambalo litaweza kukiendeleza Chama hicho.
Amesema Napenda kuwaona viongozi wanaowajibika
kiujasiri na watendaji katika chama,kitu ambacho kitaweza kupiga hatua nzuri katika
chama amesema.
Vilevile amekishauri Chama kutengeneza
mbinu mbadala ya kuweza kuleta mapato sambamba na kinamama kuazisha miradi ya na
vikundi vya ushirika katika jimbo hilo
na kuweza kujitegemea kiuchumi.
Ziara ya wajumbe wa Kamati ya Siasa
ya Mkoa wa Magharibi kwa wilaya ya Mfenesini imeanza januari 15,mwaka huu ilimalizia
mwishoni mwa wiki hii katika jimbo la bububu , ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Magharibi
Yussuf Mohammed Yussuf, iliyoanza kutembelea jimbo la Dole, Mtoni na Bububu kwa lengo
la kuimarisha Chama cha Mapinduzi katika Mkoa huu.
Hongera Mwakilishi wangu, nadhani wengine waige mfano wake, umeonesha njia kwa kuanza kutekeleza ahadi zako. Nadhani sasa tufike wakati tumchaguwe mtu kwa kigezo cha kutekeleza ahadi zake, usiwe na wasiwasi kwa staili hii utakuwa muwakilishi wetu wa kudumu hatuna cha CUF wala CCM, sisi wengine hatuangalii chama ila utendaji wa kiongozi mwenyewe.
ReplyDelete