Habari za Punde

Sipka wa Baraza la Wawakilishi Azinduwa Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi.



SPIKA  wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho (katikati) akizinduwa Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi, kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Profesa  Peter Chris Maina,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar na kulia Balozi wa Norway  Tanzania Ingunn Klepsvik, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi mdogo wa Baraza la Wawakilishi Chukwani jana 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho kulia akimkabidhi nakala ya Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho kushoto akimkabidhi nakala ya Kitabu  Balozi Norway Nchini Tanzania. Ingunn Klepsvik,
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho kushoto akimkabidhi nakala ya Kitabu Balozi Mdogo wa India Zanzibar.
  Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho kulia akimkabidhi nakala ya Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi Profesa Peter Chris Maina Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini  Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, akishughudia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakimsikiliza Spika Pandu Ameir Kificho, akihutubiwa wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Elimu ya Katika kwa Wananchi, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi mdogo wa baraza huko Chukwani Zanzibar. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Pandu Ameir Kificho, akihutubia wakati wa uzinduzi wa Kitabu cha Elimu ya Katika kwa Wananchi. kulia Balozi wa Norway Tanzania na kushoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar. Profesa Peter Chris Maina, kutoka Kituo cha Sheria Zanzibar ni mmoja wa washiriki wa kukianda Kitabu hicho, akitowa maelezo wakati wa uzinduzi wake katika Ukumbi wa Mdogo wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.
Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar akitowa maelezo wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi. 
  Mwakilishi wa Jimbo ra Hahaleo Nassor Salim Jazira na Mwakilishi wa Kwahani  Ali Salum Haji, wakiwa makina kusikiliza hutuba ya Mhe Spika akizindua kitabu hicho.
Waheshimiwa wakisoma Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi.
Wajumbe wakipitia kurasa za Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi
Wadau wa Kituo cha Sheria Zanzibar wakipitia Kitabu cha Elimu ya Katiba kwa Wananchi wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.