Habari za Punde

Mwanza vurugu tupu



Na Mwandishi wetu
VURUGU kubwa zimetokea jijini Mwanza kati ya polisi na waendesha bodaboda.

Vurugu hizo zilianzia katika mtaa wa Mission barabara iendayo uwanja wa ndege wa Mwanza.

Ghasia hizo zimeibuka baada ya polisi kuanzisha operesheni ya kuwasaka na kuwakamata waendesha bodaboda wasio na leseni na helmeti.

Waendesha bodaboda wanapiga operesheni hizo zinazofanyika nyakati za usiku ambapo bodaboda kadhaa wamekamatwa.

Vurugu zilipozidi, polisi walilazimika kutumia risasi za moto na mabomu ya machozi kuwatawanya bodaboda hao ambao walikuwa wamefunga barabara ya kuelekea uwanja wa ndege kwa kutumia mawe.


Watu walikuwa wakikimbia ovyo kuwekwa moshi wa mabomu ambao ulihanikiza eneo lote la kuelekea uwanja wa ndege.

Vurugu hizo zilisababisha huduma za usafiri kusimama kwa takribani masaa mawili.

Kamanda wa polisi mkoani humo, Arnest Mango alisema polisi itaendelea kukabiliana na boda boha hao na kamwe hawawezi kuogopa.
Polisi imethibitisha kuwakamata watu wanane watu wanane kuhusika na vurugu hizo.

Aidha askari polisi wawili walijeruhiwa kwa mawe wakati wakikabiliana na waandamanaji hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.