Habari za Punde

Sizini watakiwa kulitumia soko la Jumapili

 
Na Masanja Mabula, Pemba
NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zahra Ali Hamad amewataka waajasiriamali katika Shehia ya Sizini Pemba kuongeza juhudi za kuzalisha bidhaa zenye ubora ili waweze kujitangaza na kunufaika na kazi zao.
Alisema tatizo kubwa linalokwamisha bidhaa zao kupata soko ni ukosefu wa elimu ya kuhifadhi bidhaa na kuwataka kushirikiana na viongozi wao wa jimbo kutafuta mwalimu wa kuviendeleza vikundi hivyo.
Akizungumza na wanaushirika wa vikundi vya kuweka na kukopa katika shehia hiyo alisema serikali iko pamoja nao ili kuona bidhaa zao zinapata soko la ndani na nje ya Pemba.
Aidha aliwashuri viongozi wa vikundi hivyo kulitumia soko la Jumapili lililoanzishwa katika mji wa Chake Chake kwa ajili ya kwenda kuuza bidhaa zao jambo ambalo alisema huenda likafungua milango kwa bidhaa zinazotoka Sizini kupata soko la uhakika.
"Soko la Jumapili lipo, litumieni kwa kupeleka bidhaa zenu , hii ni fursa yenu kuweza kupata soko la kuuzia bidhaa mnazozalisha, na hii pia itasidia kupata wageni wa kuja kununua bidhaa hapa hapa kwenu," alishauri.
Mapema katika risala yao wanavikundi hao wamemwambia Naibu waizri huyo, vikundi hivyo vina zaidi ya shilingi milioni 14 ambapo tayari mikopo 9 yenye thamani ya shilingi 7,476,000 imetolewa kwa wanachama.
Aidha amezitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni pamoja na ukosefu wa vitendea kazi ikiwemo vifaa vya kutengenezea sabuni, upikaji wa mafuta ya nazi , vyeherehani pamoja na mashine ya kusukumia maji kwa wanakiundi wa kilimo cha mboga mboga.
Naibu waziri huyo ameahidi kuwapatia vyerehani viwili vya sinja pamoja pampu ya kusukumia maji ambapo naye Mkurungezi wa Elimu ya Maandalizi na Msingi Uledi Juma Wadi ameahidi kuwapatia cherehani moja ili kuunga nguvu juhudi za wanakikundi hao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.