Habari za Punde

Maafisa bandarini wadaiwa kuiba tanzanite. Dk.Mwakyembe aagiza wakamatwe


Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
WAZIRI wa Uchukuzi Dk. Harrison Mwakyembe ameagiza kukamatwa maafisa kadhaa katika Bandari ya Dar es Salaam kutokana na kutuhumiwa kuhusika katika wizi wa madini ya tanzanite kutoka Rwanda.

Dk. Mwakyembe alisema katika kipindi cha miezi minne serikali imekuwa ikipokea malalamiko kutoka serikali ya Rwanda juu ya wizi wa madini hayo unaofanywa katika bandari hiyo.

Hatua ya Waziri huyo ni muendelezo wa mkakati wake wa kuisafisha bandari hiyo ambayo imekimbiwa na wafanyabiashara wengi kutokana na kuwepo  ufisadi.

Hivi karibuni Waziri huyo alimfukuza kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA) pamoja na wasaidizi wake kutokana na utendaji mbovu na ubadhirifu uliosababisha serikali kukosa mapato.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.