Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akikata utepe kufungua zawia ya Tumbatu Jongowe,alipohudhuria katika maulidi ya Mtume Muhamad (SAW) yanayosomwa kila mwaka katika kijijini hapo
Baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu wa Tumbatu Jongowe na Vijiji Jirani walioalikwa katika maulidi ya Mtume Muhammad (SAW) wakiwa katika zawia ya kijijini hapo palipofanyika Maulid hayo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(kushoto) akitia ubani kuyafungua Maulid ya Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika jana Tumbatu
Jongowe,alipohudhuria akiwa mgeni rasmi,(kulia) Kadhi Mkuu Sheikh Khamis Haji
Baadhi ya Akina Mama wa Tumbatu Jongowe na Vijiji Jirani walioalikwa katika maulidi ya Mtume Muhammad (SAW) wakiwa nje ya zawia ya kijijini hapo palipofanyika Maulid hayo
Mwanafunzi Mhadi Haji Vuai, wa madrasa Nurmunawar ya Tumbatu Jongowe akisoma maulid ya Mtume Muhammad (SAW) mlango wa kwanza yaliyofanyika jana katika zawia ya kijijini hapo
Wanafunzi wa madrasatul Maamur ya Tumbatu Jongowe wakisoma Qaswida wakati wa maulid ya Mtume Muhammad (SAW)yaliyofanyika jana katika zawia ya kijijini hapo
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa pili kushoto) akitiliwa marashi wakati wa kumswalia Mtume Muhammad (SAW),yalipofanyika Maulid huko Tumbatu Jongowe jana,alipohudhuria akiwa mgeni rasmi,pamoja na viongozi na waumini mbali mbali wa Dini ya Kiislamu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi maalum kutoka kwa mwanafunzi Mohamed Haji Mohamed,iliyotayarishwa na wazee wa Tumbatu Jongowe wakati wa Maulid ya Mtume Muhammad (SAW),yalipofanyika jana.
[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
KATA YA MABOGINI YAPOKEA FEDHA BILIONI 15 YA MIRADI YA MAENDELEO.
-
NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
KATA ya Mabogini iliyopo katika Jimbo la Moshi vijijini Halmashauri ya
Moshi mkoani Kilimanjaro imepokea fedha Bilioni 15 kwa ajili...
46 minutes ago
ndugu zangu hakuna haja ya kuwaalika wanasiasa kwenye sherehe kama hizi , ni kizitia dosari buree , kwani wao hukualikeni kwenye sherehe zao ? si husheherekea peke yao na kupewa mafungu ya fedha kwa ajili hio. Msipoteze muda wenu kuwaalika watu ambao hamna uhakika nao kuhusu uadilifu wao.
ReplyDeleteHukumu ya Huyu iko kwa Allah, kajifanya kama kuwasahau Masheikh wetu aliowatia kizuizini na kuwatesa, Sisi Wananchi tuko pamoja na wafuasi wa Allah sio yeye Shein na kumualika mtu kama huyu na kumkenulia meno ni kujifanya wanafiki mbele ya Allah.
ReplyDeleteHuyu kakubali kuweka Sera za Chama juu na kutii mamrisho ya Chama na sio ya Allah, Furaha na misiba imewakuta Mashekh wetu wakiwa ndani kama vile wamesahaulikana.
Kwa kweli inaskitisha!...sisi wangetutolea angalau yule Mselemu Ally tu huyo Faridi tena hata kama watamfunga maisha shauri yao!
ReplyDelete