Habari za Punde

MKURUGENZI MKUU WA UNESCO AWASILI ZANZIBAR KWA ZIARA YA SIKU MBILI.

 Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova (mbele katikati)akiwasili Zanzibar kwa ziara ya Siku mbili kwa ajili ya kutembelea sehemu za Mji mkongwe na kukutana na Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Ardhi,Makaazi,Maji na Nishati, Habari Utamaduni Utalii na Michezo pamoja na Waziri wa Ustawi wa Jamii Maendeleo ya Wanawake na Watoto,hapo Serena Hotel Zanzibar.

  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali  Ali Juma Shamhuna akimpokea Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.ambaye atakuwapo  Zanzibar kwaZiara ya siku Mbili  kutembelea maeneo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar
Mkurugenzi Mkuu wa Unesco Irina Bokova akisalimiana na Viongozi mbalimbali waliokuja kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Zanzibar,ambaye atakuwapo Zanzibar kwa Ziara ya siku Mbili  kutembelea maeneo ya Mji Mkongwe wa Zanzibar

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.