Habari za Punde

Mkutano wa wawakilishi, viongozi na madiwani Kaskazini Pemba

  Baadhi ya Vitambulisho ambavyo vimeachwa katika Ofisi za Vitambulisho Kisiwani Pemba ambovyo Wenye hawakujitokeza kuchukuwa Vitambulisho hivyo na kubaki kwa muda mrefu..
Mkurugenzi wa Idara ya Vitambulisho Zanzibar Mohammed Ame Juma, akiwaonesha Wabunge Wawakilishi na Madiwani Vitambulisho ambavyo Vimekuwa katika Ofisi za Vitambulisho Pemba katika Mikoa ya Kusini na Kaskazini bila ya Wenyewe kujitokeza kuvichukuwa vikiwa vimekaa kwa muda mrefu.
Hali halisi ya Vitambulisho vikiwa vimekaa kwa muda mrefu katika Ofisi za Vitambulisho Kisiwani Pemba bila ya wenyewe kujitokeza kuvichukuwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,Dadi Faki, akifunguwa Mkutano wa Wawakilishi na baadhi ya viongozi wa Shehia na Madiwani kujadili suala la Vitambulisho vya Mzanzibari huko Wete.
 Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Mzanzibari, akieleza jambo kwa Wawakilishi, Masheha na Madiwani juu ya Vitambulisho. huko Pemba.

Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo, ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Gando, akieleza jambo juu ya Upatikanaji wa Vitambulisho vya Mzanzibari mkaazi huko Wete, Pemba.
 Waziri Wa Nchi Ofisi Rais na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Mwinyihaji Makame, akieleza jambo kwa Wawakilishi, Masheha na Madiwani , juu ya suala zima la mashirikiano katika kazi.

 Baadhi ya Madiwani wa Wilaya ya Chake Chake Mkoani na Micheweni wakisikiliza maelezo kwa Mkurugenzi wa Vitambulisho na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Mblm, huko Pemba , Juu ya kufanya kazi kwa Mashirikiano.
Naibu Katibu Mkuu Wa Cuf, Hamad Massoud , akitowa rai juu ya Ugawaji Wa Vitambulisho Vya Mzanzibar Huko Mkoani Pemba.Picha zote na Bakari Mussa Pemba

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.