Na
Kauthar Abdalla
AFISA
mradi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kutoka shirika la Action
Aid, Nadra Subeit Ali amesema mafunzo ya lugha za alama kwa askari polisi yana umuhimu katika utendaji wa
kazi zao kwani yatapunguza masuala ya ukatili wa watoto.
Akizungumza
na mwandishi habari mara baada ya mafunzo hayo katika ukumbi wa elimu mbadala
Rahaleo, alisema kumekuwa na matukio mbali mbali ya ukatili kwa watoto viziwi
na hali ambayo inapelekea kukosekana kwa ushahidi.
Alisema
watoto wenye ulemavu hufanyiwa mambo ambayo hayastahiki kufanyiwa katika jamii
lakini jambo la kusikitisha wanashindwa kwenda kuripoti katika vituo vya polisi
kutokana na tatizo la mawasiliano.
Aidha
alisema malengo makuu ya kuandaliwa mafunzo hayo kwa askari ni kuwafanya wawe
karibu na waathirika wa vitendo hivyo kwani ndio wanaopokea kesi kwa mara ya
kwanza na kushindwa kuwasiliana nao.
Alifahamisha
kuwa watajitahidi kutafuta kila mbinu ili kuhakikisha watu wenye ulemavu hasa
wa vziwi wanapata haki zao za katika sehemu mbali mbali ikiwemo katika vyombo vya
sheria.
Nae
Mkuu wa Dawati la jinsia polisi Madema, Zahor Faki Mjaka alisema mafunzo ya
lugha kwa askari yana umuhimu kwa sababu ya wateja wanaowapata huwa wana
mahitaji maalum na wanashindwa kuwasiliana nao hadi watafute wakalimani kutoka
sehemu nyengine.
No comments:
Post a Comment