Na Mwashamba Juma
SERIKALI
ya Mapinduzi ya Zanzibar na serikali ya Oman
jana zilizindua mradi wa Ushirikiano wa Elimu ya juu wa Sultan Qaboos (SQAF)
kupitia njia ya mtandao.
Mradi
huo unaojumuisha udhamini wa masomo ya juu, uliozinduliwa na Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar, Ali Juma Shamuhuna akishirikiana na Waziri wa Elimu
ya Juu wa Oman, Dk. Rawya Saud Al- Busaid utaaza mapema mwaka wa masomo 2013-2014.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Waziri Shamuhuna alisema Zanzibar itahakikisha mradi
huo unafika mbali kama ilivyokusudiwa na serikali mbili hizi, na kusema kuwa
kuzinduliwa kwa Mradi SQAF kunaimarisha urafiki uliopo baina ya Zanzibar na Oman.
Aidha
aliishukuru serikali ya Oman kwa kukichagua Chuo Kikuu Cha Zanzibar (SUZA)
katika kutekeleza mradi wake huo na kuongeza kuwa Zanzibar inaelewa umuhimu wa elimu
katika viwango vyote.
Kwa
upande wake Waziri wa Elimu wa Oman,
Dk. Busaid alisema mradi SQAF ni muhimu katika kuendeleza maendeleo ya kiuchumi
na jamii pamoja na kukuza tamaduni za nchi mbili hizo.
Dk.
Rawya alisema kuzinduliwa kwa mradi huo kutaboresha mahusiano mema hasa katika
nyanja ya elimu baina ya Oman
na Zanzibar,
sambamba na kurudisha historia ya nyuma baina ya nchi mbili hizi kwa kuendeleza
ushirikiano wao wa wa kindugu uliodumu kwa muda mrefu.
Aidha
alisema mradi pia utachangia kukuza maendeleo ya SUZA na kuzidisha thamani
kubwa ya chuo hicho.
Mfuko wa
elimu ya juu wa Sultan Qaboos (SQAF) unatarajiwa pia kutoa taaluma kwa ngazi ya
shahada ya kwanza, shahada ya pili na shahada
ya uzamivu (PhD) katika fani za elimu, afya, mazingira, miundombinu na ujasiriamali.
Hata
hivyo, Dk. Rawya alisema mbali na Zanzibar kunufaika na mradi wa (SQAF) pia
mradio huo umezishirikisha nchi 10 kutoka bara la Amerika, Ulaya, Asia na
Afrika zikiwemo Marekani, Uingereza, Poland, Malta, Uholanzi, Ujerumani, Australia,
Finland, Malaysia na Afrika Kusini.
No comments:
Post a Comment