Habari za Punde

Dk Shein aendelea na ziara yake Mkoa wa Kusini Unguja

Na Rajab Mkasaba, Ikulu
 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameendelea na ziara yake katika mkoa wa Kusini Unguja na kuwaeleza wananchi kuwa Serikali anayoiongoza itahakikisha inawapelekea huduma muhimu ya maji safi na salama pamoja na kuendeleza ujenzi wa nyumba za maendeleo Mpapa.
Dk. Shein alieleza hayo kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake katika Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja alipokagua ujenzi wa mradi wa tangi la maji Machui unaondeshwa kwa jitihada za Serikali kutokana na mkopo wa Benki ya Afrika (ADB) pamoja na kuangalia ujenzi wa nyumba za maendeleo Mpapa.
Wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Machui mara baada ya ukaguzi wa ujenzi huo, Dk. Shein alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imechukua juhudi za makusudi za kutafuta fedha kwa ajili ya kuwaondoshea wananchi wake tatizo la maji safi na salama.

Alisema kuwa tatizo la uhaba wa kuwepo kwa maji safi na salama ni tatizo la maeneo mengi ya hapa Zanzibar na ndio sababu kuu iliyoipelekea serikali kuchukua juhud hizo za makusudi ili wananchi wapate kufaidika na huduma hiyo muhimu.
Dk. Shein alisema kuwa mradi huo utaondosha tatizo sugu la maji linalowakabili wananchi wengi hasa katika maeneo ya Wilaya ya Kati vikiwemo vijiji vya Mgenihaji, Uzini, Kitumba na maeneo mengineyo ya karibu.
Alisema kuwa tangi hilo la maji litawanufaisha wananchi wapatao 31 elfu mradi ambao utahusiha pamoja na uchimbaji wa visima katika maeneo mbali mbali.
Nae Mkurugeni mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), Dk. Mustafa Ali Garu alisema kuwa mradi huo wa maji safi na salama ni miongoni mwa miradi ambayo inaendeshwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutokana na mkopo wa zaidi ya Tsh. Bilioni 67.
Alisema kuwa mradi huo unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa mwaka ujao ambapo mbali na mkopo huo serikali nayo inachangia kiasi maalum cha fedha
Wakati huo huo, Dk. Shein alifika katika kijiji cha Mpapa kuangalia hatua za ujenzi wa nyumba za maendeleo unaoendelea kijiji hapo.
Katika maelezo yake Dk. Shein alielez kuwa Serikali ya Mapnduzi Zazibar itahakikisha inaendelea kuwajengea wananchi wake makaazi bora ila pale hali itakaporuhusu.
Alisema kuwa kutokana na Zanzibar kukabiliwa na changamoto ya ongozeko la watu nalo limepelekea kuwepo kwa uhaba wa huduma muhimu kama vile maji na hata makaazi..
Dk. Shein aliwahakikishia wananchi wa Mpapa kuwa jingo hilo litakamilishwa na kupewa wananchi.
Alisisitiza kuwa kutokana na maombi ya nyumba hizo yaliyoombwa na wananchi alisema kuwa wananchi wanaoishi mjini hawatopewa nyumba hizo hata wakiwa na asili ya vijiji katika eneo hilo, hiyo ni kutoa nafasi kwa wananchi wa maeneo hayo pekee.
Alisema kuwa kupitia Wizara husika itafanya uchambuzi mkubwa wa mgao wa nyumba hizo ili kuhakikisha wanaopewa ni wale wananchi wenye matatizo na mahitaji hayo na wale wanaokaa katika vijiji husika.
“Nyumba ya mjini inatosha hata kama unakaa nyumba ya kukodi”, alisema Dk. Shein.
Alisema kuwa serikali haidharau shida za wananchi na ndio maana imekuwa ikichukua jitihada hata kukopa fedha ili iwahudumikie wananchi kwani hivi sasa serikali zote mbili inakopesheka.
Dk Shein pia, aliwataka wananchi kuendelea kutoa michango yao katika kuendeleza huduma na miradi ya kimaendeleo na kutoa pongezi kwa Uongozi wa Wizara ya Ardhi, Maji, Waziri waMakaazi, Ujenzi na Nishati, Mwakilishi wa Jimbo la Uzini pamoja na mafundi wa nyumba hiyo.
Aidha, Dk. Shein aliwaahidi wananchi wa kijiji hicho cha Mpapa kuendeleza kituo hicho cha afya pale kilipofikia. Pamoja na hayo, aliitaka Wizara husika kuhakikisha hitilafu zilizopo katika jingo hilo zinafanyiw akazi ili imalizike na hatimae apewe wananchi wakae.
Nae Katibu Mkuu wa Wizara hiyo alieleza kuwa majengo hayo yaliopo Mpapa ambayo ni mawili oja lilijengwa na kumalizika mwaka 1968 hadi 1971 na jingo la pili lilianza kujengengwa mwaka 1974 na ndipo mnamo mwaka 2004 Serikali ikaamua kuendeleza ujeni wa jingo hilo jipya lenye nyumba 24 sawa na lile la zamani.
Alisema kuwa gharama za ujenzi zilizotumika kwa jingo hilo kuanzia mwaka 2010/2011 hadi 2012/2013 zimeshafikia milioni mia mbili na hamsini na tatu, 253,000,000.
Alisisitiza kuwa fedha hizo zimetolewa na Serikali ya Mapinduzi anzibar kwa kuendeleza miradi ya maendeleo.
Wakati huo ho Mwakilishi wa Jimbo hilo alikabidhi vifaa vya miundombinu ya maji yenye zaidi Tsh. Milioni 11 huku akiahidi kuendelea kutoa mchango wake katika kuwapelekea wananchi wa Jimbo lake huduma ya maji safi na salama katika vijiji vyote kwa awamu hasa vile vyenye ukosefu mkubwa wa huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.