A,alaikum! Habari Mr Othmani, napenda kuchukua nafasi hii ili niweze basi na mimi kukupa pongezi na shukurani za kipekee kabisa kutokana na juhudi zako binafsi na za kujitolea muda wako wa msingi katika kutupatia habari na matukio mbali mbali yanayotokea huko nyumbani Zanzibar.
Kwa kweli hatuna budi kukutia moyo zaidi katika hili kwani sisis tulio nje ya Zanzibar huwa tunafurahi saaana tupatapo matukio ya habari iwe kwa maandishi au picha kwani hujiona kama tuko huko wakati tunasoma au kuangalia picha.
Saivi nipo hapa Dar kidogo basi nimeona bora nikupongeze ndugu yangu kwa hilo. Na la pili ilikua ni ombi langu tu kuwa utuongezee kutuchangamsha na football letu la ZNZ kwa kutupatia matokeo na habari kadiri iwezekanavo (frequent updates) maana tunafurahi mno sisi Wazanzibari tuliolipenda SOKA letu la Zanzibar.
La mwisho, pia ni maoni yangu pamoja na wazanzibari wengine hapa tunakiomba kwa namna moja au nyengine kwa vile wewe ni mwandishi wa habari ulieko huko nyumbani basi tunakuomba vilevike utupatie angalau VICHWA vya habari kuu vya magazeti ya Zanzibar kama vile Zanzibarleo nk maana tunatafuta internet ila hatuyaoni.
Kwa kweli bila ya kukuficha kitu tunakutegemea wewe katika kupati habari mbali mbali za huko nyumbani.
Shukrani sana Othmanimapara kwa blog inayotuhusu. God provide with you His Blessings.
Hongera sana kwa kumtia moyo bwana Mapara.
ReplyDeleteHata mimi napata faraja kubwa kupitia mtandao huu, kwa zanzibar ni mtandao wa kwanza ambao unatupa habari za kijaamii, na upi update, shukurani sana Bwana Othman mapara.
ReplyDeleteTunaomba sana sana utupatie sana habari za kijamii pia, kama mazingira, matukio ya kijamii,kuona miji wetu wa zanzibar na maendeleo ambayo tunayoletewa na yanayopotea.
Pia tunakuomba katika matukio ya jamii, kwa mfano hapo juu tumeona miji michafu na kutuwekea picha halisi, ukipata wasaa uwe unapitia wizara husika kuhoji na kupata majibu na kutuwekea hapo katika ukurasa, hio itasaidia kwetu kupata taarifa kamili nasi kuwasilina na vyombo husika.
Mdau Ghalib kutoka UK.