Habari za Punde

Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF Awataka Wananchi kuwa Makini

Na Khadija Khamis –Maelezo Zanzibar 7/03/2013
Mjumbe wa Baraza Kuu la CUF.Juma Duni Haji amewataka Wazanzibar kuwa makini katika mchakato mzima wa Katiba Mpya.

Hayo aliyasema leo huko katika uwanja wa mkutano magogoni wakati akiwahutubia wananchi wa jimbo hilo .

Alisema kuwa wazanzibar wakae pamoja kuweza kutafakari kupata katiba iliyobora wao na vizazi vijavyo

Aidha alisema katiba mpya itakuwa ina nguvu na ndio katiba mama hivyo wananchi wasikubali kutumiwa na watu wachache kwa masilahi yao .

“tunataka nchi yetu kama iliyokuwa 1964 yenye mamlaka yake kamili alisema Babu Duni.
Aidha alisisitiza kuwa wazanzibar lazima watetee nchi yao kwanza na Dunia itaheshimu maamuzi ya wananchi ambayo wanayataka .

Alisema kuwa Masheha wa shehia mbali mbali wawe walimu kwa wananchi ili kuelimisha wananchi wao isiwe ni miongoni mwa kuwapotosha .

Duni aliwataka wananchi kusimama kidete kuokoa nchi yao ambayo wao wameridhi kwa wazee wao na wao waweza kuwasaidia virembwe na vijukuu vyao ili kuikuta na kuweza kuitumia nchi hii ya Zanzibar

Alisema kuwa wasikubali kutekwa nchi yao iwe huru na yenye mamlaka kamili nje na ndani ya nchi bila ya kuingiliwa na nchi nyengine

Nae Mbunge wa Jimbo la Magogoni Hamad Ali Hamad ameeleza kuwa ataendeleza kutekeleza ahadi zake mbali mbali alizoahidi yeye pamoja na mwakilishi na diwani katika kuiletea maendeleo jimbo lao la magogoni .

Alisema katika ahadi hizo baadhi wamekwisha zitekeleza ikiwemo kuwapatia wananchi maji safi na salama kujenga madarasa mbali mbali .kuvichangia vikundi mbali mbali vya akinamama na kadhalika

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.