Wazazi jana ilibidi kuchukuwa tahadhari za Watoto wao kutokana na mvua ilionyesha na kusababisha ajali ya kufariki kwa mtoto, Wazazi walifika maskulini kuwachukuwa watoto wao ili kuepusha madhara kwao, kama inavyoonekana mzazi huyu akiwa na mtoto wake akipita katika moja ya sehemu iliotokea ajali ya kuzama kwa mtoto na kupoteza maisha.
Mpanda baskeli akipita kwa tabu katika barabara ya Kariokoo kwenda Miembeni ikiwa barabara hiyo imejaa maji ya mvua ilionyesha na kusababisha hali hiyo na kuleta usumbufu wananchi, baada ya muda wa kumalizika kwa mvua hiyo maji yamepungua na kurudi katika hali ya kawaida na kupitika bila ya taabu.
No comments:
Post a Comment