Habari za Punde

Mvua za Masika Zasababisha Kifo cha Mwanafunzi wa Darasa la Kwanza

Askari wa Kikosi cha Zimamoto Zanzibar wakiwa katika jitihada za kuutowa mwili wa Mwanafunzi Munaifaty Abdalla Yussuf (8) wa Skuli ya Kijitoupepo, aliyeteleza katika mtaro wa maji katika barabara ya kwenda fuoni eneo la kijitoupele
Askali wa Kikosi za Zimamoto wakiwa katika jitihada za kuutafuta mwili wa mtoto Munifaty Abdalla Yussuf,(8) aliyezama katika eneo la kijitoupele, leo asubuhi akati akienda skuli.

Wananchi wakiwa na huzuni wakati wa zoezi la kuokoa mwili wa marehemu aliyefariki kutokana na kuingia katika eneo la kijitoupele akienda skuli asubuhi leo wakati mvua ikinyesha na kusababisha ajali hiyo.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo watoto hao walikuwa wawili wakipita eneo hilo  wameshtushwa na honi ya gari ya daladala iliokuwa ikiwapita na ikabidi kusogea pembeni na wote wawili wakateleza katika eneo hilo na mmoja alijitahidi kutoka na kutaka kumuokoa mwenzake akashindwa kutokana na nguvu ya maji yaliokuwa yakipita katika mtaro huo ukikatisha barabara,
 
Jitihada za wananchi zilishindikana kuuopoa mwili huo uliokuwa umeganda katika mtaro huo na kikosi cha zimamoto wakachukua jitihada za kuchimba sehemu ya pili ya barabara hiyo na kuupata mwili huo.  

 Gari la Kikosi cha Zimamoto Zanzibar likiwa katika eneo la tukio
Gari la Wagonjwa la Kikosi cha Uokozi Zanzibar likiondoka sehemu ya tukio baada ya kufanikiwa kuupata mwili wa mwanafunzi wa darasa la kwanza wa skuli ya Kijitoupele, baada ya kuteleza na kuingia katika mtaro huo ulioko katika barabara ya kwenda fuoni eneo la kijitoupele Zanzibar.

 Wananchi wakiangalia sehemu uliotolewa mwili wa Mwanafunzi wa Darasa la Kwanza wa skuli ya Kijitoupele , baada ya kuteleza na kuingia katika mtaro wa maji na huku mvua ikinyesha na kusababisha kuchukuliwa na maji na kuvutwa katika mtaro huo na kusababisha kifo chake, wakati akienda skuli asubuhi leo.na Picha ya chini ni eneo aliloteleza  na kuingia katika mtaro huo katika eneo hilo wananchi wakiangalia baada ya kutolewa. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.