The PBZ Managing
Director, Mr Juma Amour Mohamed
Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ
Ltd) ambayo ni benki pekee yenye makao makuu yake Zanzibar na ambayo inamilikiwa
mia kwa mia na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekuja na huduma mpya yenye
kuwawezesha Watanzania wanaoishi nje kuleta pesa nyumbani Tanzania kwa bei nafuu
kuliko wanavyolipia hivi sasa kupitia kampuni za nje za kigeni za
kutuma pesa.
Katika waraka ambao blog la
Zanzibar Ni Kwetu umeuona, benki hio inawataarifu wana-jumuia wa
Diaspora ya Watanzania huko Canada juu ya huduma hio na wanawataka wawajulishe
Watanzania wengine wote wanaoishi nje, ili na wao wapate
kufaidika.
Katika kufanikisha huduma hii Benki ya
Watu wa Zanzibar inashirikiana na kampuni moja maarufu kutoka Uingereza
inayoitwa World Remit ambayo Benki ya Dunia (World Bank) inaielezea kwenye
website yake kuhusu remittances kuwa bei zake za kutuma pesa kutoka nchi moja
kuenda nyengine ni nafuu.
Kwenye waraka huo Benki ya Watu wa
Zanzibar inamuandikia rasmi Communication Director wa Zanzibar-Canadian
Diaspora Agency (ZACADIA) Bw. H.S. Othman wa Toronto, Canada, kuwa,..."We
are therefore kindly asking your Agency in the Diaspora to pass the message
contained in this letter to all Tanzanians abroad, so that they could use the
services of our local indigenous bank in Tanzania,...."
Mwakilishi
wa Zanzibar Ni Kwetu kutoka Toronto, Canada, alilinganisha
bei ya huduma hii kwa kutaka kupeleka Tanzania viwango tofauti vya pesa kutoka
Canada kupitia huduma ya PBZ/World
Remit na kampuni nyengine ya Western Union. Tofauti
aliyoiona kama alivyoiwakilisha hapa chini itawastaajabisha wengi wanaowaletea
jamaa zao na ndugu zao pesa kutoka nje.
AMOUNT FROM CANADA TO TANZANIA
($)
|
FEES CHARGED BY ONLINE REMITTING
COMPANIES ($)
| ||
PBZ /WORLD
REMIT
|
WESTERN
UNION
| ||
1.
|
Up to 50.00
|
3.99
|
5.00
|
2.
|
50.00 –
75.00
|
5.99
|
12.00
|
3.
|
75.00 –
100.00
|
6.99
|
12.00
|
4.
|
100.00 –
150.00
|
7.99
|
20.00
|
5.
|
150.00 –
300.00
|
9.99
|
25.00
|
6.
|
300.00 –
500.00
|
11.99
|
30.00
|
7.
|
500.00 –
600.00
|
12.99
|
30.00
|
8.
|
600.00 –
995.00
|
13.99
|
40.00
|
Huduma hii yenye bei nafuu inapatikanwa
online kwa nchi zote za European Union, Canada, Australia, New Zealand, etc na
karibuni itapatikanwa katika USA.
Benki ya Watu wa Zanzibar inayo matawi
tisa katika Tanzania nzima - mawili yakiwa mjini Dar Es Salaam na karibuni
itafungua matawi mapya katika mji wa Mtwara na Mwanza, huku ikilenga kuwa na
tawi katika kila jimbo la kule Bara.
Huduma hii ya kupeleka
pesa inapatikanwa online kwenye address ya hapa chini:
Benki ya Watu wa Zanzibar inawashauri
Watanzania wanaoishi nje kuitembelee hii site na kujiandikisha hata kama hawana
nia ya kupeleka pesa nyumbani hivi karibuni. Ukijiandikisha mapema itakusaidia
wakati wa dharura!
No comments:
Post a Comment