Habari za Punde

Tutunze Mazingira ya Mitaa yetu kwa Usafi.

 Wadau wangu kutunza mazingira ni jukumu la kila Mtu na jamii kuweka mazingira safi katika sehemu za makazi yetu ili kuepuka na miripuko ya maradhi, na kuchukuwa jitihada za makusudi kuhimiza vyombo husika kufuata utaratibu wake wa kuondoa taka katika majaa, ikizingatiwa wakati huu ni wa mvua za masika zimeanza kunyesha inaweza kusababisha maradhi kwa jamiii inayokaa karibu na sehemu za kutupia taka.Inahitaji kuchukuwa hatua za haraka kuondoa mrundikano wa taka katika majaaa yetu ili kuuweka mji wa Unguja katika mazingira Safi Mtu ni Afya.

2 comments:

  1. Hii hatari kwa kweli viongozi wa nchi hii hawawezi lolote kwasababu mfumo mzima uliokuwepo wa serikali, wahusika wa manispaa, naona huyu Meya wa mara hii sijui kama anafanya kitu kazi yake kwenda ikulu ikiwa kuna shughuli za kuapisha viongozi na Rais akisafiri ndio anaonekana, huu mfumo wa umeya kuchaguliwa katika madiwani lazima ubadilike bila ya hivyo kila siku tutapata vichwa maji

    ReplyDelete
  2. Kitu ambacho kinacho niuma kodi yangu ninayo lipa inafika mfukoni mwa viongozi, budget zinazotolewa na serikali hazitumiki ipasavyo, hapo katika hiyo picha naona ni kwamba sio kosa la wananchi bali ni wizara ya manispaa, wameshindwa kuja kuchukua hilo tagi lao na kwenda kutupa hizo taka, ikiwa maendeo ya mjini kama michenzani yako hivyoo jee huko uswahili maendeo ya nje ya mji utakuwaje ?

    Ikiwa serikali haina magari ya kusafishia miji kwa nini wanashindwa kuomba misaada, fedha wanapewa katika budget yao zinafanyika kwa kitu gani ? Kodi wanazokusanya kutoka kwetu zinaenda wapi ?

    Inaniuma sana sana, wallah viongozi wanaturudisha nyuma, hawa hasa wakurugenzi, na hao wakilishi wetu wako jamaniii hawaoni halii hii, mimi nilivyo sikia ni kwamba hata hao wakilishi wetu au mawaziri wetu hasa upande wa upinzani hawasikilizwi, kwa vile hawa wakurugenzi ndio watendaji wakuu katika mawizara ni viburi kwa vile wao wameweka na jamaa zao viongozi fulani ,wanatoka chama fulani...


    Hatutafika kweliii.

    Mji wetu mdogo sana, mimi kama ningekuwa na wizara hii zanzibar ingenukia perfum, wallah tena, sitaki uwaziri nataka ukurugenzi niwe mtendaji mkuu, wallah nafukuza mutu yoteee inayoleta upumbavu.

    Nakuomba mwandishi kama utapata muda pita kwa mtendajiii, au muakilishi wa jimbo hilo na kuhojii, shukurani.

    Pia katika mtanadao wako mbona hatuoni shemu ya kuona habari zilizo pita ? Muhimu

    SHUKRANI

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.