Kuna baadhi ya Wananchi hufanya kwa makusudi kuhakatika maeneo mbalimbali bila ya kujali athari zake kutokana na uchimbaji wa mchanga huo kwa kipato cha mara moja bila ya kujali athari yake kwa jamii na vizazi vijavyo.
Angalia hali hii watu hawa hawajui umuhimu wa mazingira ya maeneo yao au ni makusudi tu. Nguzo hii ya Umeme mkubwa ikiwa iko katika hali ya wasiwasi kutokana Wananchi hao kuchimba mchanga katika eneo hilo lililopita nguzo za umeme mkubwa katika maeneo ya kwarara. ikizingatiwa wakati huu wa mvua za masika zinaweza kuleta madhara kwa nguzo hiyo na kuhatarisha amani ya wananchi wa eneo hilo.
Watu kama hawa taassisi husika inabidi kuchukuwa jitihada za makusudi kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria kukomesha vitendo vya uvunjaji wa sheria
No comments:
Post a Comment