Habari za Punde

Waziri Mbarouk afanya uteuzi wa Mrajis wa vyama vya Michezo


Waziri wa Habari, Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar, Said Ali Mbarouk amefanya uteuzi kwa kumteua Mrajis wa michezo na mjumbe mmoja wa Baraza la Michezo Zanzibar.

 Katika uteuzi huo, Waziri Mbarouk amemteua Said Malik Juma kuwa Mrajis wa vyama vya michezo ambaye atashika nafasi hiyo kuanzia leo.

 Said Malik Juma ambaye ni Mwanasheria katika Wizara ya Habari, Utamaduni Utalii na Michezo ni mwanataaluma wa sheria akiwa na shahada mbili za sheria.

 Aidha Waziri Mbarouk amemteua Uledi Juma wadi kuwa mjumbe wa baraza la michezo Zanzibar.

 Uledi Juma ni Mkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Maandalizi na Msingi anashika nafasi iliyoachwa wazi na Mussa Abdulrabbi kutoka Wizara ya elimu na mafunzo ya amali ambaye alijiuzulu hivi karibuni.

 Imetolewa na idara ya hHbari Maelezo Zanzibar 27/03/2013

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.