WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais, Fatma Alhabib Ferej, amesema watu wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto kubwa ya elimu ndogo inayochangia kukosa ajira seriakalini huku wemgine wakishindwa kuomba nafasi hizo za kazi.
Alisema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Amani, Fatma Mbarouk Said, alietaka akujua kama kuna mpango maalum wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu kuweza kusoma na kuwapatia mikopo na ruzuku ili wafikie malengo.
Akijibu hoja hiyo, Waziri Fatma alisema serikali kupitia sheria ya utumishi wa umma inalazimisha mtu kuomba kazi inayolingana na sifa za kielimu alizonazo pale inapotangazwa lakini changamoto kubwa inayojitokeza ni elimu kwa kundi hilo.
Alisema sheria hiyo pia imekuwa ikitoa unafuu kwa watu wenye ulemavu kwani wapo watu waliowahi kuajiriwa kupitia sheria hiyo ingawa chanagamoto hiyo ya ajira iko kwa Wazanzibari wote.
Alisema suala la ajira kwa watu wenye ulemavu linahitaji mipongo ya muda mrefu.
Alisema katika kukabiliana na hali hiyo, serikali bado imekuwa ikitoa ajira hizo kwa wale ambao hujitokeza kuomba kwa kuzingatia elimu yao na pia kupitisha upendeleo maalum kwa kundi hilo inapoona inafaa kufanya hivyo.
Mfano halisi Waziri huyo alisema Tume ya Utumishi ilishawahi kutoa ajira ya kutaka mtu mwenye shahada ya kawanza, lakini alieomba alikuwa ni mtu mmoja aliyekuwa na Diploma, lakini walipoangaliwa aliweza kuajiriwa kutokana kwa kuwa aliyekuwa akitakiwa ni mtu mwenye ulemavu licha ya elimu yake kuwa ndogo.
Alisema mfano mwengine serikali imeamua kutoa huduma kuhakikisha watu wenye ulemavu wanasomeshwa katika madarasa ya elimu mjumuisho ili kuwawezesha kielimu.
Alisema kitendo cha jamii kuwaona watu wenye ulemavu ni watu wa kusaidiwa tu halina msingi wowote.
Hata hivyo alisema serikali haina takwimu kamili za watu wenye ulemavu, lakini kazi ya kuwahakiki imeanza.
No comments:
Post a Comment