Habari za Punde

Kutoka Baraza la Wawakilishi - Taasisi za umma zatakiwa kuanzisha vyombo kusimamia usalama kazini

TAASISI za serikali zimetakiwa kuwa na vyombo vya kusimamia usalama kazini ili kuepusha kutokea madhara makubwa.

Waziri wa Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Haroun Ali Suleiaman, aliyasema hayo jana wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Amani, Fatma Mbarouk Said, aliyetaka kujua ni hatua zipi wizara inazichukua kuwafundisha wananchi na watumishi wa umma juu ya kutumia vifaa vya kinga kazini.

Akijibu suala hilo waziri huyo, alisema, vifaa vya kinga vimekuwa vikiwekwa na wamekuwa wakivihakiki kupitia taasisi husiaka ikiwemo ya Idara ya maafa na kikosi cha uokozi kupitia kamati ya usalama kazini.

Alisema hadi sasa zipo taasisi ambazo zina vifaa hivyo na Idara ya usalama na afya kazini imekuwa ikiendelea kuwasiliana na Kamisheni ya Utumishi wa umma, juu ya kufanya utaratibu wa ukaguzi wa kina katika taasisi za serikali.

Alisema taasisi hiyo hivi sasa inakusudia kuhakikisha kila wizara ya serikali na mashirika ya umma yanakuwa na idara za usalama kazini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.