Na Abdi Suleiman, Pemba
LICHA ya kushuka dimbani ikiwa imeshateremka daraja, timu ya Mila imeibugiza Konde Star mabao 7-4 katika mchezo wa mwisho kukamilisha ligi daraja la kwanza Taifa Pemba.
Mchezo huo uliopigwa juzi uwanja wa Gombani, na kuhudhuriwa na mashabiki wachache, ulikosa ladha na timu hizo kuonekana kama zilikuwa kwenye mazoezi.
Kutokana na hali hiyo, baadhi ya mashabiki walisikika wakidai kuwa, timu hizo zilishapanga matokeo hayo.
Mabao ya Konde katika mchezo huo, yaliwekwa kimiani na Ali Khamis (dk. 13, 86), Hamza Mwalimu (dk, 27) na Hamad Omar aliyefunga mnamo dakika ya 65.
Washindi wa mchezo huo Mila, walifungiwa magoli yao na Hamad Omar Ali (dk. 38, 48 na 64,) Hamza Mwalimu (dk. 52), Simai Mussa (dk 74, 76 na Haji Hassan akihitimisha karamu hiyo katika dakika ya 84.
No comments:
Post a Comment