Habari za Punde

Mtuhumiwa wa Mauaji ya Padri Mushi Afikishwa Mahakama ya Zanzibar Leo.

 Mtuhumiwa wa Mauaji ya Padri Mushi, akitoka katika chumba cha Mahakama baada ya kusomwa kesi hiyo leo asubuhi na kurudishwa rumande mpaka tarehe 18-4-2013 kwa kusikilizwa tena.  
 Mtuhumiwa wa Kesi ya Mauaji ya Padri Mushi, yaliotokea  17-2-2013, katika maeneo ya Bertras , akiwa katika chumba cha mahakama kabla ya kuanza kwa kesi hiyo leo asubuhi. 
 Mtuhumiwa wa Kesi ya mauaji ya Padri Mushi,Omar Mussa Makame  akizungumza na Wakili wake Abdalla Juma Mohammed baada ya kusomewa kesi hiyo leo ya kutuhumiwa kumuua Padri Mushi katika Mahakama ya Vuga, baada ya kufikishwa mahakamani leo asubuhi.

6 comments:

  1. Mbona hujatueleza kitu na Leo ilikuwa lisikilizwe shauri la dhamana kwa kuwa DPP alilikataa jalada la uchunguzi kwa kuwa halikuwa na mashiko au amegeuza kibao tena kalikubali?

    Naona polisi Zanzibar wameanza tena kuwabambikizia Watu kesi kwa kuzingatia siasa nia aibu kweli kwa polisi na Serikali kwa ujumla.

    ReplyDelete
  2. Hizi Serikali za Tanzania hazina wasemaji wa Serikali? Ukimya wao, au kutokuwepo chombo hiki kinatoa fursa kwa raia kujaza mwanya huu na kusababisha kuleta utata katika masuala muhimu ya nchi. Hebu wahusika ama wadau chemsheni bongo na mrekebishe kasoro hii.

    Mambo kama haya ya mauaji ni mazito na athari zake zinanaswa na mataifa mbali mbali na kuathiri heshima na sifa ya nchi yetu. Kuweni na utaratibu mzuri wa kutoa habari hasa masuala ya kistrategia kwani kimya chenu ni sumu kwa taifa.

    Kwa mfano, tunaambiwa FBI wameondoka kimya kimya, mara wameshirikiana na vyombo vyetu kuwasaka wauaji wa Padri, leo tumeskia hawakuhusishwa na utata unazidi kuendelea.Zindukeni.

    ReplyDelete
  3. Ama huu ni uonevu,kubabikizwa mtu asiye husika kesi kwa ajili ya siasa,mbona hao FBI hawakukamata mtu?wakaondoka kimya kimya?,mwenyezi mungu amesha ahidi kila anae mdhulumu mwenziwe malipo huanza hapa hapa duniani na akhera fenar jahannam,wameuana wao kwa wao mnampandikiza mtu mwengine.

    ReplyDelete
  4. Ama kweli ukafiri unafanya kazi,!!!!!!!!!!Hata wewe mapara unazi block comet za watu kwa ajili wanalaumiwa CCM wenzio?ok tutakutana kwaboko,nyinyi ndio mnao turudisha nyuma nchi esiendele,Kwa uwezo wake mwenyez mungu ZNZ tutakomboka tu.

    ReplyDelete
  5. Anony wa nne hakuna comments iliyokuwa blocked hapa.

    Uwezo kuziblock comments tunao kwa comment yoyote ya matusi au ya kuchafua hali ya hewa.

    Ila tumeweka uhuru wa kila mmoja mwenye maoni yake yawe ya kupongeza , kukosoa , kurekebisha ana rukhsa ya kufanya hivyo ndio maana hatujaanza kumoderate comments.

    ReplyDelete
  6. huyu jamaa wanamtesa na kumdhulumu tu kwavile wamekosa lakujibu kwa mabwana zao nchi za magharibi hususan marekani ndo wakaamua wamtoe mhanga raia asonahatia ili kujipendekeza zaidi.... na nakupongeza zanzibar news blog yako haibagui habari tofauti na zengine hasa mzalendo sometimes wanaeka pumba badala kutetea zanzibar wanatetea cuf bila kujua cuf na ccm ndo haohao tu politicians they are there for their own benefits with their families.. zanzibar zinduka

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.